
Mabasi ya Abiria yakiwa yamepaki stand
Wakizungumza na Lindiyetu.com kupitia Katibu wa Muungano wa vyama vya Madereva Bw. Rashid Saleh, madereva hao wamesema kuwa suala la kurudia kusoma ni aina nyingine ya unyanyasaji kwa maelfu ya madereva nchini, ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa hawana mfumo mzuri wa ajira licha ya kutupiwa lawama kibao kuwa wao ndio chanzo cha ongezeko la ajali nchini.
Katibu huyo wa Muungano wa Vyama vya Madereva ameitaja kero nyingine kuwa ni hatua ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT kutamka hadharani kuwa vyeti walivyonavyo madereva hao sio halali na kwamba Ijumaa wiki hii wanakusudia kukutana na Waziri wa Kazi na Ajira kwa ajili ya kuzungumzia kero hizo kwa lengo la kuepusha kutokea kwa mgomo huo.
Tags
HABARI ZA KITAIFA