Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi WILLIAM LUKUVI
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi WILLIAM LUKUVI ametoa siku 30 kwa maafisa wa ardhi na watendaji mkoani DSM kuhakikisha wanashughulikia na kutafuta ufumbuzi wa kero mbalimbali za ardhi jijini humo.
Akizungumza na maafisa watendaji kutoka Manispaa za TEMEKE, ILALA na KINONDONI Waziri LUKUVI amesema Manispaa ya KINONDONI inaongoza katika migogoro ya ardhi ambapo amesema wakazi wake wanakabiliwa na shida kubwa hasa katika upimaji wa viwanja.
Waziri LUKUVI amewataka watendaji wa sekta hiyo kushiriki kikamilifu kutatua matatizo mbalimbali yanayowakabili wananchi hususani kwenye sekta hiyo.
Katika kukabiliana na tatizo hilo, amesema serikali inatarajia kuanza kutumia mfumo mpya wa usimamizi wa rasilimali ardhi unaojulikana kama Land Management System utakaotumika katika usimamizi, upimaji, upangaji, utoaji wa hati pamoja na kufichua udanganyifu unaofanywa na baadhi ya maafisa wa wizara hiyo.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.