Unknown Unknown Author
Title: WAATHIRIKA WA MAFURIKO SHINYANGA WAFUNGA BARABARA WAKISHINIKIZA SERIKALI IWAPATIE CHAKULA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Baadhi ya waathirika wa mafuliko katika kijiji cha mwakata wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga jana walilazimika kuifunga barabara ya Isaka- ...
Baadhi ya waathirika wa mafuliko katika kijiji cha mwakata wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga jana walilazimika kuifunga barabara ya Isaka- Kahama na kuathiri kwa muda mawasiliano katika nchi ya Rwanda,Burundi na Uganda....
wananchi
Wananchi  hao walifanya  vurugu  hizo  ili  kuishinikiza serikali kuwagawia chakula,magodoro,branketi, mahema na shuka baada ya kunyeshewa na mvua usiku wakati vifaa vya misaada vikiwa vimefungiwa kwenye maghala hali iliyosababisha jeshi la polisi kuwatawanya wananchi kwa mabomu ya machozi na kufungua njia ili gari ziendelee na safari.
  
Vurugu hizo  zilidumu kwa  muda  wa saa moja ambapo kundi la wananchi wenye hasira walisikika wakiilalamikia kamati ya maafa kwa kushindwa kuwahudumia waathirika kwa wakati hali iliyosababisha waathirika wanaolala nje kunyeshewa mvua. 

Kufuatia vurugu hizo mbunge wa jimbo la msalala Mh.Ezekiel Maige alilazimika kufika  eneo la tukio na kujionea hali halisi ambapo aliwasihi wananchi kuwa watulivu wakati akifanya mipango ya kuzungumza na kamati ya maafa ili iweze kutoa vifaa vinavyolalamikiwa na vigawiwe  kwa walengwa.

Alipotakiwa kujibu malalamiko hayo, katibu wa maafa Wilaya ya Kahama ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ushetu Kahama Bi.Isabela Chilumba alisema vurugu hizo zinasababishwa na wanasiasa na kwamba kamati ya maafa imebaini kuna  kundi la vijana kutoka  vijiji jirani wamekuwa wakivizia chakula na vifaa vya misaada.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top