Unknown Unknown Author
Title: TAARIFA YA MWENYEKITI LINDI PRESS CLUB
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Abdulaziz Ahmeid Mwenyekiti wa Lindi Press Club Habari za muda huu wanahabari wenzangu,waratibu,wazeshaji na ma T.A wakiwemo wahasibu...
Abdulaziz Ahmeid Mwenyekiti wa Lindi Press Club
Abdulaziz Ahmeid Mwenyekiti wa Lindi Press Club

Habari za muda huu wanahabari wenzangu,waratibu,wazeshaji na ma T.A wakiwemo wahasibu

Naitwa Abdulaziz Ahmed, ni mwandishi wa habari wa kituo cha runinga cha cha channel ten, Ambae pia ni mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari wa mkoa wa Lindi.

Lakini kwa Nyongeza mimi ni mbunge mtarajiwa wa jimbo la Lindi mjini na bado kidogo tu Akina Hassan Simba na Group lake la Chawaku mtanibadilisha na kuniita Mheshimiwa mheshimiwa. Naomba Mniunge Mkono na Dua Zenu..

Binafsi nisingependa niwe Mwezeshaji katika kikao kazi hiki Kwani kazi hiyo imekwisha kufanywa na wawezeshaji kwa umahiri na kwa ufanisi mkubwa.

Pia washiriki tulipata nafasi ya kuchangia na kubadilishana uzoefu na hatimae tutaondoka na mikakati kamambe ya kuiunga mkono serikali katika mpango wake huu wenye nia njema na adhimu kwetu kama taifa.

Kama ilivyolezwa hapa kwamba suala la kupambana na umaskini lisihusishwe na itikadi za vyama vya siasa wala dini na hata kabila wala rangi na jinsia ya mtu.

Kwani umaskini upo kwa watu ambao wapo kwenye makundi hayo bila kuchagua.

Hivyo niwajibu wetu kuunga mkono juhudi hizi kupitia kalamu zetu. Niwashukuru kwa sana TASAF na serikali kwa ujumla wake kwa kutambua sisi waandishi wa habari kama ni sehemu ya mafanikio ya mpango ikiwa tutashirikishwa kikamilifu katika mpango huu.

Niwahakikishie tu kwamba tutoa ushirikiano uliotukuka na wenye tija kwa jambo hili. Kwa kuwa Watu wameskini wana kila sababu ya kukwamuliwa kutoka katika hali hiyo ili nao waweze kutoa mchango wao katika maendeleo ya kiuchumi kwa taifa na miaka ijayo kwa faida ya vizazi vijavyo.

Tumejifunza na kufundishwa mengi na wawezeshaji kama nilivyotangulia kueleza.Naomba Nikiri tu kwamba mengi ya yale niyojifunza nilikuwa siyajui kabla ya kikao kazi hiki.Nahali ingendelea kuwa hivyo bila shaka ningekuwa ni miongoni mwa watu ambao wangeandika kinyume na hali halisi au upotoshaji.

Nashukuru nimewezeshwa uelewa mapema kabla ya kuharibu.Nimejifunza kuwa kumbe ushirikishwaji unaofanywa katika kuwapata walengwa,yaani kaya maskini una faida kubwa.Ili kuepuka viongozi kuteua watu,jambo ambalo lingesababisha kuingizwa kaya zisizo na sifa kwa sababu binafsi hasa za kimaslahi.Hali ambayo ingezua malalamiko na migogoro na kusababisha nia ya kuzifikia kaya million 1 kukwama.Kwani muda mwingi ungetumika katika kutatua migogoro.Lakini kwa mfumo na muundo uliopo katika kuwatambua walengwa ni mzuri sana hasa unapoanzia katika ngazi za vitongoji.Ambapo mapendekezo hayo yanapelekwa katika serikali za vijiji na hatimae mikutano mikuu ya vijiji utaratibu unaofanywa Kwa haki

kabla ya kupata mafunzo haya niliamini kuwa huo ni urasimu usio na sababu za msingi.Ndugu zangu,uongo ukirudiwa kila mara unaweza kubalika na kufanywa ukweli ingawa kiuhalisia uongo unabaki kuwa uongo japokuwa utakuwa umeanza au umeaminiwa nakuanza kuitwa ukweli.

Gharama ya kufuta uongo ni kubwa sana,nadhani niwajibu wetu sasa tukaporudi tukasaidie kufuta uongo uliopata kuzungumzwa au unaozungumzwa na utakao zungumzwa kuhusiana na mpango huu.Kama tulivyosikia kwamba fedha zinazotumika katika kufanikisha mpango huo zinatolewa na shirika la wajenzi huru yaani free mason ambayo inanasibishwa na shetani(devils or satanic).Nilikuwa sijui kuwa miradi hii ni ya jamii na TASAF niwawezeshaji tu.Kwani wanaoibua hiyo miradi ni wanajamii wenyewe kutokana na vipaumbele na changamoto zilizopo kwenye maeneo yao.Naamini si mimi tu bali ni wengi kama sio wote walikuwa wanaamini kuwa miradi hii ni mali ya TASAF na kwa hiyo tukajikuta kuwa ni washiriki namba moja wakuilamu TASAF na baadhi yetu kudiriki kuandika habari potofu ama kwa kutoelewa au kwa utashi na sababu binafsi za mwandishi.Naamini baada ya kupata elimu hii hatutaweza kufanya makosa ya aina hiyo.Na atakaye fanya atakuwa ameshindikana kama ambavyo jiwe linavyoshikana kuiva kwakuchemshwa kwenye maji ya moto.

Sio wajibu wangu kutoa ushuhuda wa mafanikio yaliyopatikana katika mpango huu kwa kaya maskini. Lakini japo kwa uchache niweze kutoa mfano. NI Hivi juzi tu Ikiwa ni siku moja kabla ya kuanza kikao kazi hiki mimi na mwandishi mwenzangu anayeandikia gazeti la RaiaTanzania. Tulikwenda wilayani Kilwa na kutembelea vijiji na kuzungumza na walengwa. 

Hakika mimi na mwenzangu hatukuweza kabisa kuamini mafanikio ya mpango huu wilayani humo. Watu wengi wametoa ushuhuda usio na chembe ya shaka kwamba mpango huu umewanufaisha sana. Wengi wao wameanzisha miradi, hasa ya ufugaji kuku na mbuzi kupitia fedha za mpango huu.

Yupo mtoto ana umri wa miaka 14 yupo darasa la nne hana mama wala baba (marehemu) anaishi na dada yake tu ambaye pia ni mdogo. Lakini sasa kupitia mpango huu anasoma bila mashaka na anapata milo yake kwa wakati. Kilichotufanya tusiamini, Bila kuficha ni kwamba mimi na mwenzangu tuliamini tungekuta changamoto nyingi ambazo zingesababisha mpango huu kutofanikiwa. Nijambo ambalo hata mratibu na T.A wa wilaya ya Kilwa ambao walikuwa ni wenyeji wetu hupata ugumu wa kazi zao kuogopa kuazimiwa na madiwani ambao kila kukicha wanawakataa watendaji. 

Kubwa zaidi ni hofu ya kuwepo changamoto zinazotokana na mivutano ya kisiasa iliyopo katika wilaya ya kilwa. Hali ambayo ilitufanya tuamini kwamba ushindani wakisiasa umewaingia wanajamii na kuingiza mpango huu katika ushindani huo na kuathiri mpango huu. Lakini hali nitofauti kabisa, mambo ni shwari. Sielewi wahusika wa mpango huu wametumia njia gani zilizosababisha mafanikio hayo ktk eneo lenye changamoto hiyo. Majibu wanayo wenyewe lakini mimi mwenyewe na kwaniaba ya mwenzangu tunawapongeza sana.

Wakati nakaribia kufika mwisho wa hotuba yangu nisingependa nimalize bila ya kuwakumbusha wanahabari wenzangu kuona haja ya kuyafanyia kazi kwa vitendo haya tuliyojifunza. Mimi siamini kama serikali imeamua kutuwezesha fedha tu sisi waandishi wa habari na kuwa ni kama au miongoni mwa kaya maskini wanazozihudumia, la hasha. Bali ni kwa lengo na makusudio maalum kama ilivyoelezwa na wawezeshaji hasa mkurugenzi Wa Tasaf alipokuwa akifungua juzi..Ni jambo lisilopendeza na lisilofaa na kwa jumla ni aibu kuondoka hapa tukiwa vichwa vitupu na kuacha mafunzo haya katika ukumbi huu. 

Tumeanza kuona ni jinsi gani wengine walivyoshiriki na wengine tulivyohudhuria. Wapo walioshiriki na tulio hudhuria. Kila mtu atajua mwenyewe kama yupo kundi gani kati ya makundi haya mawili. Nawaomba Tukatoe ushirikiano stahiki katika maeneo yetu kwani mikoa hii ni miongoni mwa mikoa maskini sana na sisi wengi wetu ni wakazi au wazawa wa maeneo ya mikoa hii na Tuwe sehemu ya mapambano haya, tusipotoshe jamii bali tuwe waelimishaji. Tuwe ni sehemu ya wasuluhishi pale inapotokea migogoro na changamoto. 

Mfano mdogo tu ambao niliwahi kushuhudia vurugu ambayo nusura itutie aibu mbele ya wageni ambao ni wafadhili wan chi hii waliokuwa wamewakilisha mashirika mbalimbali ikiwamo Worldbank,,ILO, UNDP na mengine walikuja kushuhudia utekelezaji wa mradi huu. Ilikuwa pale katika kijiji cha Kiwalala wakati wa kulipa fedha kwa kaya maskini. Nilikuwa na waandishi mwenzangu. Mbele ya wafadhili na watendaji wa TASAF makao makuu wengine mupo hapa mnakumbuka, baadhi ya wananchi kwa makusudi walianzisha vurugu zisizo na kichwa wala miguu. Sababu kubwa walikuwa wanadai zoezi lilifanyika kwa upendeleo na kwamba fedha zile ni kwa ajili ya wazee wote.

Lakini walipoulizwa hatua zilizotumika kuwatambua walengwa walikiri zilifuatwa zote. Hata hivyo baadhi yao walikuwa hawaelewi kwani walihusisha mpango huo na itikadi za siasa. Ilibidi sisi waandishi tufanye kazi ya ziada kuthibitisha kuwepo na mikutano ya kuwapitisha wanaolipwa na ushahidi ninao. 

Tulifanikiwa kutuliza munkari na mambo yalikwenda sawa. Ndivyo tunavyotakiwa kuwa. Kama tusingekuwa makini basi zile vurugu ingekuwa ni stori ya kuchomoka nayo katka TV Au magazeti. Mwisho kabisa nitumie fursa hii kuwaaga rasmi kwa nafasi yangu ya uenyekiti wa Lindi Press Klabu ambayo nimekuwa kiongozi kwa miaka 7. Kwani katika uchaguzi ujao tutakaofanya JULY sitogombea Nafasi yangu. Maana kama nilivyotangulia kueleza kwamba natarajia kuomba ridhaa ya wanachama wa CCM LINDI ili wanichague kugombea ubunge wa jimbo la Lindi mjini.

Nitaendelea kushirikiana nanyi kama mwandishi wa habari na kushiriki kikamilifu katika mapambano haya ya kuondoa umaskini uliopo miongoni mwetu

Ahsanteni sana kwa kunisikiliza.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top