Unknown Unknown Author
Title: SONGA'S YAJITOLEA KUINUA KIWANGO CHA ELIMU KATIKA WILAYA YA RUFIJI NA KILWA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Shirika la kutoa misaada ya kielimu la READ INTERNATINAL , limefanikiwa kukarabati chumba cha maktaba na kutoa msaada wa vitabu na samani ...
Shirika la kutoa misaada ya kielimu la READ INTERNATINAL, limefanikiwa kukarabati chumba cha maktaba na kutoa msaada wa vitabu na samani katika shule ya sekondari ya Kilwa, mkoani Lindi.
READ INTERNATINAL
Akikabidhi katika hafla ya ufunguzi wa maktaba hiyo iliyofanyika Kilwa masoko mwishoni mwa wiki iliyopita. Mwakilishi wa shirika hilo ambaye ni miongoni mwa vijana waliojitolea kusimamia na kuratibu ukarabati huo, Flavian Emmanuel. Alisema shirika hilo kwa ufadhili wa kampuni ya SONGAS liliona kunaumuhimu mkubwa wa ukarabati wa chumba hicho na kusaidia vitabu vya kiada na ziada ili wanafunzi wa shule hiyo waondokane na tatizo la vitabu.
Maktaba Kilwa day
Alisema shirika hilo limetekeleza mpango huo katika wilaya za Rufiji na Kilwa. Ambapo katika shule hiyo licha ya kurabati chumba hicho na kusaidia vitabu vya ziada na kiada 1400, lakini pia limekabidhi meza na kuzitengeneza meza na viti vilivyokuwa vimeharibika. 

Mwakilishi huyo ambaye yeye na wenzake niwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar-es-salaam. Aliushauri uongozi wa shule hiyo umtafute mkutubi mwenye sifa ili aweze kuendesha maktaba hiyo kwa ufanisi.
Maktaba Kilwa day
Naye mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa, Maimuna Mtanda alisema taasisi, mashirika na wahisani wa maendeleo wanawajibu mkubwa wa kuitupia jicho sekta ya elimu, kwani ni msingi wa maendeleo ya taifa lolote duniani.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top