Unknown Unknown Author
Title: SIRI NZITO YAFICHUKA!!..NI KUHUSU MATUMIZI yA VIUNGO VyA ALBINO!!!...SOMA HAPA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Matukio ya mauaji ya watu wenye ulemavu ya ngozi yanaendelea kujitokeza nchini, ni wiki moja baada ya mtoto mmoja Yonana Bahati kuuawa G...
Alibinisim
Matukio ya mauaji ya watu wenye ulemavu ya ngozi yanaendelea kujitokeza nchini, ni wiki moja baada ya mtoto mmoja Yonana Bahati kuuawa Geita na watu wasiofahamika na leo kuna mlemavu mwingine ameripotiwa kukatwa mkono huko Sumbawanga.

Leo kwenye Power Breakfast Clouds FM, kulikuwa na mazungumzo na Mkurugenzi wa shirika linalotetea haki za watu wenye ulemavu wa ngozi la Under The Same Sun, Vicky Mketema, amezungumzia jinsi ukatili huo unavyofanyika;

“Watu ambao wanataka madini ule mguu wanasema kwamba unakuwa kama ni chombo cha kuangalia madini yako wapi katika mwamba.. wanachokifanya ni kwamba huu mguu unapelekwa katika eneo na kuna kelele ambazo zinatokea wanazozisema wao kama vile kelele za kwenye redio wakati unatafuta stesheni, kwa hiyo iyo kelele inapotokea ndipo ambapo mganga anawaambia kwamba anze kuchimba"

"Anaweza kuambiwa achukue damu ambayo awe amekuja nayo au ni mganga kampatia lakini pia ni damu ya binadamu, lazima kafara ya binadamu itolewe ile damu sasa mganga anasema kwamba anaimwaga katika eneo moja halafu ule mchuruziko wa damu ndio unaofuatwa pale ambapo hiyo damu itatuama katika huo mchuruziko basi ndipo hapo huyu mtu wa madini ataambiwa kwamba anza kuchimba katika eneo hili“


Vicky Ntetema

Vicky Ntetema
“..wakati mwingine wanasema kwamba wanapoishiwa viungo wanawaomba wenzao.. kuna muungano wa waganga wa kienyeji ambao wanatumia viungo vya watu wenye Albinism anapoishiwa hapa anamuomba mwenzake Kijiji cha pili au kama sio Kijiji cha pili anakwenda hata nchi jirani, hayo yote ni maneno yanayosemwa na waganga wenyewe ” maelezo ya Vicky Mketema.

Mtetema amesema nywele za albino pia huwa zinakaangwa na kutumiwa na wavuvi kuvuta samaki kwenye maji.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top