Unknown Unknown Author
Title: MUME WA ZAMANI WA MSICHANA ALIYEZAA NA CHRIS BROWN ACHIMBA MKWARA MZITO..!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mume wa zamani wa msichana aliyezaa na Chris Brown amechimba mkwara kuwa kama muimbaji huyo akiendelea na hasira zake mbele ya familia yake...
Mume wa zamani wa msichana aliyezaa na Chris Brown amechimba mkwara kuwa kama muimbaji huyo akiendelea na hasira zake mbele ya familia yake ataingia kwenye matatizo makubwa na yeye binafsi.
CHRIS NA NIA
Mtandao wa TMZ umeongea na Terry Amey – anayesema kuwa alimuoa Nia kuanzia mwaka 2003 – 2014 na wana mtoto pamoja wa kike mwenye miaka 13 aliyedai kuwa ndio maana anataka Chris ajue kuwa hatanii.

Terry anasema alitengena na Nia baada ya kupata mimba lakini kwakuwa alijua kuwa haikuwa mimba yake aliamua kumpa talaka. Anadai hakuwa anajua kuwa mtoto huyo ni wa Chris.

Amey ameuambia mtandao huo kuwa anajua jinsi Chris alivyo mtu wa hasira na anasema ni bora ajizuie akiwa karibu na Nia na watoto wake ama kutakuwepo na madhara makubwa.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top