Kiungo kutoka nchini Rwanda, Haruna Niyonzima amesema hatomuomba radhi yoyote ndani ya klabu ya Dar es salaam Young Africans, kufuatia kadi nyekundu aliyoonyeshwa jana wakati wa mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara uliowakutanisha na mahasimu wao Wekundu wa Msimbazi Simba.
Niyonzima, alionyeshwa kadi nyekundu na muamuzi Martin Saanya, baada ya kuupiga mpira wakati kipyenga cha muamuzi huyo kikiwa kimeshapulizwa kwa kuashiria Ivo Mapunda alikua amechezewa ndivyo sivyo na Amis Tambwe.
Niyonzima, amesema atakuwa mpuuzi kama atamuomba radhi yoyote ndani ya klabu hiyo kutokana na kuamini kwamba hakufanya kosa hilo kwa makusudi na ndio maama mara baada ya kuadhibiwa kwa kadi nyekundu alikua akimsisitizia muamuzi hakusikia kipyenga.
“Sitomuomba radhi yoyote na sioni sababu ya kufanya hivyo, japo ninatambua nimeigharimu sana yanga, lakini si kwa hatua ya kumpigia magoti mtu kwa kigezo cha kuonyeshwa kadi nyekundu” Alisema kiungo huyo aliyepachikwa jina la Fabregas
Kiungo huyo pia amekubaliana na kichapo walichokipokea kutoka kwa Wekundu wa Msimbazi Simba cha bao moja kwa sifuri lililofungwa na Emmanuel Arnold Okwi katika kipindi cha pili.

Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.