Unknown Unknown Author
Title: TIMBWILI TIMBWILI:: MAMA WEMA AMZABA VIBAO ASKARI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mama wa Staa wa Bongo Movies,Wema Sepetu anadaiwa kumzaba vibao askari wa kampuni binafsi.  Kwa mujibu wa shuhuda watukio zima, tukio hi...
Mama WemaMama wa Staa wa Bongo Movies,Wema Sepetu anadaiwa kumzaba vibao askari wa kampuni binafsi. 

Kwa mujibu wa shuhuda watukio zima, tukio hilo lililovuta hisia za watu wengi lilijiri kwenye Bandari ya Dar es Salaam, majira ya mchana Ijumaa iliyopita. Awali ya yote shuhuda huyo alihojiwa kama s kama anamjua vizuri mama Wema ambapo alithibitisha kuwa ni yeye huku akisapotiwa na wenzake waliokuwa wakisikika kwenye simu.

“Nani asiyemjua mama wa staa mkubwa kama Wema? Tena kafuatana na Wema mwenyewe. Kila mtu hapa anamjua ngoja tujaribu kupata picha zake nzuri,” alisema shuhuda huyo kwa kujiamini.
Shuhuda huyo alidai kwamba chanzo cha yote, mama Wema alidaiwa kutumia mlango usio sahihi na alipofuatwa kuelekezwa ndipo likaibuka timbwili zito.

“Kinachoonekana alikuwa ameshuka kwenye boti akitokea Zanzibar kwenye shughuli binafsi. Wakati anatoka kuchukua hamsini zake akiwa na Wema, wakapita mlango ambao siyo sahihi.
“Sasa askari wa kampuni binafsi akawafuata na kuwazuia ili kuwapa maelekezo lakini mama Wema alikasirika, akaanza kumpiga vibao.

“Hapo ndipo lilipoibuka timbwili zito kwani askari naye hakutaka kukubali kirahisi.
“Naye mama Wema kuonesha si mtu wa mchezo aligeuka mbogo na kusababisha watu kushindwa kuamini.

“Baadaye walipelekana kwenye kituo cha polisi cha pale bandarini wakamalizana lakini tayari ishu hiyo ilishageuka gumzo maeneo hayo.“Hatujui walikubaliana nini zaidi ya kuwaona wakitimua zao kwani hawakutaka kukusanya tena watu,”
alidai shuhuda wetu huyo.

Baada ya kumwagiwa tukio hilo la moto, chanzo cha habari hii kilimtafuta mama Wema ambaye hakukanusha kutokea kwa tukio hilo badala yake aliomba aachwe kwanza apumzike nyumbani kwake, Sinza-Mori jijini Dar.
“Niache nipumzike kwanza nitakusimulia tukio,” alisema mama Wema.Alipotafutwa kwa mara nyingine hakuwa tayari kutoa ushirikiano hivyo jitihada za kusikia upande wake zinaendelea.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top