KOCHA WA MANCHESTER UNITED KUBWAGA MANYANGA KAZI YA UKOCHA

Kocha mkuu wa klabu ya Manchester United Louis van Gaal ametangaza kustaafu kufundisha mpira pindi atakapomaliza mkataba wake wa kuitumikia klabu ya Manchester United.
Luis Van Gaal
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 63 ana mkataba wa kuifunza Manchester United hadi mwaka 2017.

Mholanzi huyo amesema hana mpango wa kuendelea na fani hiyo kwani muda wake uliobaki anahitaji kuwa na familia yake.
Van Gaal amewahi kuzifunza timu kadhaa barani Ulaya zikiwemo Barcelona, Bayern Munich na Ajax.

Akizungumza kwenye mahojiano yake na gazeti la daily Telegraph amesema umri wake umeenda na kwasasa anafikiri kustaafu ukocha baada ya kumaliza kibarua chake Old Trafford maana anahitaji kuwa karibu na mke wake, watoto wake na wajukuu zake.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post