HAYAWI HAYAWI SASA YAMEKUWA..... ZITTO KABWE AJIUNGA NA CHAMA CHA ACT, ANGALIA MAPOKEZI YAKE

Zitto Rasmi ACT
Licha ya kusemwa sana kwa muda mrefu juu ya kuhusishwa na chama kipya cha siasa cha ACT-Tanzania dhidi ya aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Ruyagwa Kabwe (pichani juu akisaini kitabu baada ya kupewa kadi) sasa yamekuwa kweli kwa Mbunge huyo baada ya jana Jumamosi ya Machi 21, kupokelewa rasmi na chama hicho na kukabidhiwa kadi yake yenye namba 007194.
Zitto Rasmi ACT
Hili limetokea siku moja tu baada ya Zitto kutangaza kuachia ubunge na kuandika barua rasmi ambapo sasa amekuwa mwanachama wa ACT-Tanzania na kuahidi kuendeleza mapambano ndani ya chama hicho.
Zitto Rasmi ACT

Zitto Rasmi ACT
ACT-Tanzania: kirefu chake ni Chama cha Alliance for Change and Transparence Makao makuu ya chama hicho yapo Kijitonyama Jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Zitto Rasmi ACT

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post