Unknown Unknown Author
Title: AZAM FC WAPANIA KUTETEA TAJI LAO, WAHAHA KUIPIKU YANGA SC
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu Vodacom, Azam FC , wamepania kuing'oa Yanga SC kutoka kileleni mwa Ligi hiyo ili wao watetee vyema Taji ...
Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu Vodacom, Azam FC, wamepania kuing'oa Yanga SC kutoka kileleni mwa Ligi hiyo ili wao watetee vyema Taji Lao.
Lindiyetu Sports News
Baada ya Mechi 18 kwa kila Timu, Yanga wapo Nambari Wani wakiwa na Pointi 37 wakifuatiwa na Azam FC wenye Ponti 36.

Timu ya 3 ni Simba yenye Pointi 32 lakini wao wamecheza Mechi 2 zaidi ya Yanga na Azam FC na hivyo kuwa nje ya mbio za Ubingwa.

Timu Meneja wa Azam FC, Jemedari Said, akiongea mara baada ya kuitungua Coastal Union 1-0, huko Mkwakwani, Tanga hapo Jumapili na kuikaribia Yanga, amesema wao wana azma kubwa ya kutetea Taji lao.

Mara baada ya kutupwa nje ya CAF Championz Ligi na El Merreikh kwenye Raundi ya Awali Mwezi uliopita, Azam FC iliamua kumtimua Kocha wao Omog na kumkabidhi Timu Msaidizi wake George Nsimbe kutoka Uganda hadi mwishoni mwa Msimu wakimpa jukumu la kuhakikisha utetezi wa Ubingwa wao.

Lakini nia ya Azam FC itakuwa na ugumu kwani Yanga chini ya Kocha Mholanzi Hans van de Pluijm akisaidiwa na Charles Boniface Mkwasa ni Timu kali mno.

Hata hivyo, Jemedari Said amepania: "Tunataka kushinda Mechi zetu zote zilizobaki ikiwemo ile na Yanga ambayo ndio itaamu nani Bingwa!"

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top