SIMBA YAPIGWA FAINI YA MILIONI 3, TOTO YAPEWA POINT ZA BURE

Kagera Sugar FC Vs Simba SC
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeipiga klabu ya Simba faini ya sh. milioni tatu kutokana na timu yake kuvaa jezi ambazo hazikuwa na nembo ya mdhamini wa Ligi Kuu, kampuni ya Vodacom wakati wa mechi yao dhidi ya Kagera Sugar.

Nayo Polisi Tabora imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa kusababisha mechi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kati yake na Toto Africans iliyochezwa Januari 14 mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kuvurugika.

Kutokana na mchezo huo kuvurugika, Toto Africans imepewa ushindi wa pointi tatu na mabao matatu.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post