MWINGINE MCHEZAJI WA SIMBA AFARIKI DUNIA

KIKOSI CHA SIMBA 2003
KIKOSI CHA SIMBA KILICHOING'OA ZAMALEK MWAKA 2003

Aliyekuwa kiungo nyota wa Simba, Christopher Alex Massawe, amefariki dunia. Alex amefariki dunia akiwa mjini Dodoma ikiwa ni baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Dada wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Mama Maembe amesema Alex amefariki dunia jana saa 3 asubuhi. Tayari taratibu za mazishi zimeanza kufanywa na imeelezwa Alex atazikwa mjini humo.

Alijulikana kwa ubora wake katika ukabaji na kuichezesha timu. Lakini pia atakumbukwa kwa kuwa mchezaji aliyepiga penalti ya mwisho iliyoivua ubingwa Zamalek na kuipeleka Simba kucheza Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika 2003, hatua ya makundi.

Christopher Alex Massawe
Christopher Alex Massawe enzi za uhai wake

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post