Unknown Unknown Author
Title: MARKET PLACE FC YAIGARAGAZA BAFANA BAFANA FC GOLI 4 - 3 (PENATI) MARA BAADDA YA KUTOKA DROO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kipa wa Timu ya Marketi Place Fc akiwa amebebwa na Mashabiki wa Timu hiyo mara baada ya Kuokoa Penalti mbili na kuifanya timu yake kuibu...
Market Place Fc Vs Baffana Bafana
Kipa wa Timu ya Marketi Place Fc akiwa amebebwa na Mashabiki wa Timu hiyo mara baada ya Kuokoa Penalti mbili na kuifanya timu yake kuibuka kidedea dhidi ya wapinzani wao Bafana Bafana kwa Goli 4-3.

Na. Mwandishi Wetu
Timu ya Marketi Place Fc yaibuka Kidedea katika Mchezo wa Pili wa Ligi daraja la Tatu Ngazi ya Mkoa dhidi ya Bafana bafana ya Rutamba kwa kuichapa Bafana Bafana Goli 4 - 3 ushindi huo umepatikana kwa mikwaju ya Penati mara baada ya Kwenda suluhu ya goli 1 - 1 katika Dakika 90 za Mchezo huo.

Mchezo huo ulikuwa Mkali na wa Ushindani mkubwa kwa kuwa timu zote mbili zilikuwa zinatafuta point tatu muhimu hii ni Baada ya mchezo wa awali kutoka suluhu 1-1.

Timu ya Bafana bafana ndio ilikuwa ya kwanza kujipatia goli la kuongoza mnamo dakika ya 1 ya mchezo huo kupitia kwa mshambuliaji wake Saidi Mbela kutokana na kupiga mpira wa adhabu ambao ulimshinda mlinda mlango wa Marketi Place Fc akishindwa kuokoa mchomo huo.
Marketi Place Fc haikufanya kosa pale ilipapata nafasi ya kusawazisha goli hilo kupitia Mchezaji wake Rocky Kate Maiko katika dakika 2, Hadi kipindi cha Kwanza kinamalizika Timu hizo zilizotoka sare.

Kipindi Cha pili kilikuwa si kizuri zaidi kwa Timu ya Market Fc kwani waliruhusu mashambulizi mara kadhaa langoni mwao, lakini Beki yao ilikuwa madhubuti na kuweza kuzuia hatari zote golini kwao.

Hadi kipyenga cha mwisho cha muamuzi kinapulizwa kuashiria kumaliza dakika 90 za mchezo matokeo yalibakia 1-1 na kupelekea upigwaji wa Mikwaju ya Penalti.

Katika Hatua hiyo Kipa wa Market Place aliibuka Shujaa wa mchezo huo kwa kuokoa Penalti mbili na kuiwezesha Timu yake kuibuka Mshindi kwa jumla ya Penalti 4 - 3.

Market Place Fc Vs Baffana Bafana
Timu zikipeana Mikono Kabla ya Mchezo kuanza kati ya Market Place Fc Vs Bafan Bafana FC katik uwanja wa Ilulu leo hii. 
Market Place Fc Vs Baffana Bafana
Saidi Mbela Akishangilia mara baada ya Kuifungia timu yake ya Bafana Bafana goli la Kuongoza Leo katika uwanja wa Ilulu katika Mchezo wa ligi daraja la tatu Ngazi ya Mkoa. 
Market Place Fc Vs Baffana Bafana
Wachezaji wa Market Place wakishangilia mara baada ya Kupata goli la Kusawazisha kupitia Mchezaji wao Rocky Kate Maiko Leo katika Uwanja wa Ilulu katika Mchezo wa Ligi daraja la Tatu Ngazi ya Mkoa 
Market Place Fc Vs Baffana Bafana
Harakati katika Mchezo huo:: mchezaji wa market Place akijaribu kumtoka Beki wa Bafana Bafana leo hii katika Mchezo wa Ligi daraja la Tatu ngazi ya Mkoa. 
Market Place Fc Vs Baffana Bafana
HATARI LANGONI:; Golkipa wa Bafana Bafana akiokoa hatari langoni mwake... 
Market Place Fc Vs Baffana Bafana
Mashabiki wa Marketi Place wakishangilia mara baada ya Kupata Goli la Kusawazisha...... 
Market Place Fc Vs Baffana Bafana
Shabiki wa Market Place akiwana kijinga cha Moto katika Goli lililochaguliwa kupigwa mikwaju ya Penalti...Tukio hili lilitokea kabla ya Mikwaju hiyo kuanza Kupigwa..... 
Market Place Fc Vs Baffana Bafana
Golikipa wa Market Place akiokoa Penalti ambayo iliipa Ushindi Timu yake hiyo.... 
Market Place Fc Vs Baffana Bafana
Mashabiki wa Market Place wakiwa wamembeba Juu Juu marabaada ya kupangua Penalt mbili na kuiwezesha Timu yake kushinda mchezo huo dhidi ya Bafana Bafana ya Rutamba leo hii katika Uwanja wa Ilulu. 
Market Place Fc Vs Baffana Bafana
Mashabiki wakiendelea Kushangilia Ushindi wa Timu ya Marketi Place katika sehemu mbali mbali za Mji.. Hawa walikuwa na Mwandishi wetu.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top