Unknown Unknown Author
Title: MARKET PLACE FC YAENDELEZA UBABE, YAINYUKA BEACH BOYS 1 - 0, LIGI DARAJA LA TATU - LINDI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Ligi Daraja la Tatu Ngazi ya Mkoa limeendelea leo hii kutimua Vumbi katika dimba la Ilulu mkoani hapa kwa Kuzikutanisha Timu mbili zenye Ma...
Ligi Daraja la Tatu Ngazi ya Mkoa limeendelea leo hii kutimua Vumbi katika dimba la Ilulu mkoani hapa kwa Kuzikutanisha Timu mbili zenye Mashabiki lukuki nazo ni Market Place Vs Beach Boys.
Market Place Vs Beach Boys
Kikosi cha Kwanza cha Timu ya Market Place kilichocheza Dhidi ya Beach Boys ndani ya Uwanja wa Ilulu Hivi leo na Kuibuka kidedea kwa Ushindi wa 1 - 0.
Market Place Vs Beach Boys
Mchezaji Hija Rajabu (wakwanza kushoto) akishangilia Goli lake na wachezaji wenzake wa Market Place Fc mara baada ya Kupata Goli hilo alilofunga kwa Mpira wa adhabu.

Ni watoto wa wauza Nyanya walioibuka kifuambele dhidi ya Watoto wa Wavuvi kwa goli Moja kwa Bila.

Bao Hilo la pekee kwa Timu ya Market Place lilipatikana Mnamo Dakika ya 76 kupitia Mchezaji wake aitwae Hija Rajabu ambaye huvalia jezi nambari 11, Goli hilo lilipatikana mara baada ya Timu ya Beach Boys kufanya rafu karibu kabisa na eneo la Kumi na nane, Bila kuipoteza nafasi hiyo Hija aliweza kupiga Freekick hiyo Nzuri na kumshinda mlinda mlango wa Beach Boys na Kutinga wavuni.

MSIMAMO WA LIGI:: Hivi sasa Timu Inayo ongoza Ligi hiyo ni Timu ya Market Place huku ikiwa Imejikusanyia Point 7  na Magoli 3 huku ikifuatiwa na timu ya Transpoter (kilwa) ikiwa na Point 4 na Magoli 4 pamoja na Stand Worious wakiwa na Point 4 na Magoli 4. Timu ya Beach Boys Inashikilia nafasi ya nne huku ikiwa na Point 4 na magoli 4, Timu ya Madsoni kutoka Mtama inashika mkia huku ikiwa haina Point ila ikiwa na goli 1.

Market Place Vs Beach Boys
Mashabi wa Timu ya Beach Boys wakiwa katika Shamra Shamra za Kuishangilia Timu yao Japo walichapwa Goli 1 - 0.

Ligi hiyo Itaendelea tena Siku ya Jumapili kwa kuzikutanisha timu za Madson Fc Vs Stand Worious mcheo utakaochezwa ndani ya Uwanja wa Ilulu Majira ya saa Kumi Kamili Jioni.

Market Place Vs Beach Boys
Huyu ni Shabiki wa Timu ya Beach Boys alipoteza Fahamu mara baada ya Market Place Fc kupata Goli la Kuongoza.  
Market Place Vs Beach Boys
Kocha Marinda akiwa haamini kilichoTokea mara baada ya Timu yake ya Beach Boys Kufungwa Goli 1 - 0 na Market Place katika Ligi daraja la Tatu ngazi ya Mkoa iliyochezwa leo hii Uwanja wa Ilulu. 
Market Place Vs Beach Boys
Mashabiki lukuki waliojitokeza leo hii uwanja wa Ilulu wakiwa wanafuatilia Mchezo huo kwa Makini 
Market Place Vs Beach Boys
Mashabiki lukuki waliojitokeza leo hii uwanja wa Ilulu wakiwa wanafuatilia Mchezo huo kwa Makini
Market Place Vs Beach Boys

Waamuzi waliochezesha Mchezo wa leo hii katika Mchezo wa Ligi daraja la tatu ngazi ya Mkoa kati ya Market Place na Beach Boys Mechi iliyochezwa katika uwanja wa Ilulu
Market Place Vs Beach Boys
Mashabiki wa Timu ya Market Place Fc wakishangilia Ushindi huo dhidi ya wapinzani wa Beach Boys

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top