Unknown Unknown Author
Title: MARKET FC YATOKA SARE DHIDI YA TRANSPORTER FC KUTOKA KILWA, LIGI DARAJA LA TATU
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Ligi Daraja La tatu ngazi ya Mkoa imeanza kutimua vumbi hapo jana katika Uwanja wa Ilulu Mkoa wa Lindi kwa kuzikutanisha Timu za Beach Boys...
Ligi Daraja La tatu ngazi ya Mkoa imeanza kutimua vumbi hapo jana katika Uwanja wa Ilulu Mkoa wa Lindi kwa kuzikutanisha Timu za Beach Boys Vs Stand Worious ambapo katika Mchezo huo hakuna alietoka kifuambele dhidi ya mwenzake, Timu hizo zilitoka na Point Moja kila Mmoja na goli moja.
market fc vs transporter fc
Benchi la Ufundi la Timu ya Market Place leo katika Mechi ya Ligi daraja la Tatu dhidi ya Transporter Fc Kutoka Kilwa
market fc vs transporter fc
Benchi la Ufundi la Timu ya Market Place leo katika Mechi ya Ligi daraja la Tatu dhidi ya Transporter Fc Kutoka Kilwa

Leo hii Timu ya Market Fc (Lindi mjini) iliikaribisha Timu ya Transporter (Kilwa) katika Muendelezo wa Ligi hiyo ambayo inasaka bingwa wa mkoa.

Mchezo wa Leo ulijawa na Heka Heaka za Hapa na Pale kwani ilionekana Timu hizo zimekamiana katika kutafuta point tatu muhimu. Timu ya Market Place Ndio ilikuwa ya Kwanza kufungua milango ya kupachika magoli mnamo dakika ya 20 ya Mchezo kipindi cha Kwanza kupitia Mshambuliaji wake machachali Mwalami kupokea basi maridadi na kuutupia Mpira wavuni huku ukimuacha Mlinda mlango wa Transporter Fc akishindwa kuokoa mchomo huo.
market fc vs transporter fc
Wachezaji wa Timu ya Market Place wakishangilia Goli mara baada ya kupata goli la Kuongoza katika Mchezo wa Ligidaraja la Tatu dhidi ya Transporter Fc ya Kilwa.

Hadi Mapumziko Market Fc 1 - 0 Transporter Fc

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi hasa Timu ya Transporter Kufanya mashambulizi mengi langoni mwa wenyeji Market Fc lakini mabeki wa timu hiyo walionekana shupavu na kuzuia kash kash hizo.
market fc vs transporter fc
TFF AIBU HII.....Refa akiwa amesimamisha Mchezo na kuanza Kukagua Mpira uliokuwa wenye ahueni angalau kuinusuru mechi hiyo kuacha kuahirishwa kutokana na Uhaba wa Mipira.

Mchezo huo uliingia Dosari kwa Muda kwa kukosekana Mpira wa akiba kwani Mipira yote iliyokuwepo Uwanjani hapo haikuwa na Upepo wa Kutosha hivyo kufanya wachezaji kulazimika kuchezea Mpira usiokuwa na kiwango kizuri cha hewa na kufanya kuharibu kabisa radha ya mchezo huo. Iliwachukua kama Dakika 25 hadi kupatikana Mpira uliona hewa ya kutosha na mechi iliendelea Vyema.

Katika Hali iliyokuwa si yakawaida Refa  aliweza kukataa goli la pili lililofungwa na Timu ya Market Fc kwa kusema Mchezaji alikuwa tayari ameotea.

Mnamo dakika ya 85 Timu ya Transporter iliweza kupata Penalt baada ya Beki wa Market Fc kujichanganya na Kuunawa Mpira huo katika eneo la Hatari na Penalt hiyo Kupigwa na Mustafa Kilala na Kuipatia Goli la kusawazisha Timu yake hiyo.
market fc vs transporter fc
Golkipa wa Timu ya Market Place akishindwa Kuzuia Penalt iliyopigwa na Mustafa Kilala wa Transporter Fc na Kuisawazzishia Timu yake

Hadi Mwisho wa Mchezo Market Fc 1 - 1 Transpoter Fc

Katika Hali isiyotarajiwa Mwamuzi wa Kati alionesha Kitendo sio cha Kiungwana cha Kupiga makofi Msichana Mmoja ambaye Jina lake halikupatikana kwa haraka, Msichana huyo alikuwa kati ya wasimamizi waliokuwa wanasimamia mapato ya Mlangoni, Haikuweza Kufahamika kwa haraka sababu za Mwamuzi huyo kumfanyia Udharirishaji Mwanamke huyo.
market fc vs transporter fc
Mashabiki wa Timu ya Market Place wakiteta Jambo mara baada ya Mpira kuisha na Kutoka sare ya Goli 1 - 1.
market fc vs transporter fc
Ulinzi uliimarishwa Mara baada ya Kipenga Cha mwisho kwani Mashabiki walitaka kuleta tabu kidogo juu ya maamuzi ya Refarii...... 
market fc vs transporter fc
Timu ya Transporter Ikiwa tayari kuanza safari ya Kurudi wilayani Kilwa ambapo Timu hiyo Inatokea.

Kesho Ligi hiyo Inaendelea kwa Kuzikutanisha Timu mbili za Beach Boys na Madison Fc

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top