Unknown Unknown Author
Title: LIGI DARAJA LA TATU NGAZI YA MKOA:: MARKET PLACE FC YATOKEA MBAVUNI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Ligi daraja la Tatu limeendelea Leo hii kwa mchezo wa pili Baada ya Mchezo wa Fungua Dimba hapo jana Kuzikutanisha Timu za Transporter FC ...
Ligi daraja la Tatu limeendelea Leo hii kwa mchezo wa pili Baada ya Mchezo wa Fungua Dimba hapo jana Kuzikutanisha Timu za Transporter FC Kutoka Kilwa na Timbaland FC kutoka Nachingwea nani Timbaland Fc iliyoibuka kidedea kwa Kuichapa Transporter Fc 1 -0.
Bafana Bafana fc Vs Market Place Fc
Wachezaji wa Market fc wakitoka kushangilia mara baada ya kupata Goli la kusawazisha

Hivi leo Dimba la Ilulu zilikutana Bafana Bafana Vs Market Fc wazee wa Best Loser kama Mashabiki pinzani wanavyo waita kwa kuwa waliweza kupenya kutoka katika hatua ya mwanzo baada ya Timu moja kujitoa mashindanoni na kufanya point za timu hiyo kutosha na Kufanikiwa kusonga Mbele.

Leo hii Mchezo huo ulikuwa wa kibabe kama ilivyo ada ya Timu mbili zinapokutana na kusaka Ushindi wa Point Tatu muhimu, Rafu za hapa na pale zilitawala lakini Pongezi kwa mwamuzi wa kati Swalehe Chakupewa kwa kuweza kuumudu Vizuri mchezo huo na kutoa haki katika kila upande.

Hadi Dakika 45 za kipindi cha Kwanza hakuna Timu iliyoona Lango la Mwenzake.


Bafana Bafana fc Vs Market Place Fc
Saidi Nyenje Mchezaji wa Bafana Bafana Akitolewa nje ya Uwanja na Kukimbizwa Hospitali kupata huduma mara baada ya kupata Jeraha kichwani kwake.

Kipindi cha Pili kilianza kwa kasi kubwa hasa kwa Timu ya Market Fc kutengeneza nafasi kadhaa za kufunga lakini Ngome ya Ulinzi ya Bafana Bafana ilionesha kuwa madhubuti kwa kuokoa Hatari zote langoni Mwao.

Mnamo dakika ya 52 Mchezaji Saidi Njenje wa Bafana Bafana alichezewa rafu mbaya na kupelekea kuumia vibaya Kichwani na Kukimbizwa Hospitali ya Mkoa ya Sokoine.


Bafana Bafana fc Vs Market Place Fc
Wachezaji wa Bafana Bafana wakishangilia Mara baada ya kupata Goli la kuongoza.

Dakika ya 79 Mchezaji Saidi Mbela aliwainua Mashabiki wa Timu ya Bafana Bafana kwakufunga goli maridadi kabisa na kufanya goli hilo kuwa la kuongoza, Kabla ya Ally Mpole kuisawazishia Timu yake ya Market Fc mnamo dakika ya 90 ya Mchezo huo.


Bafana Bafana fc Vs Market Place Fc
Wachezaji wa Market Place wakishangilia Mara baada ya kupata Goli la kusawazisha

Hadi Mwisho wa Mchezo huo Matokeo yalikuwa Bafana Bafana 1 - Market FC 1

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top