Unknown Unknown Author
Title: HUZUNI YATANDA KWA WAKAZI WA LINDI, DADA MMOJA AJINYONGA HADI KUFA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Nguo iliyotumika kuchukua Uhai wa Mwanahamisi Ismail Mkazi wa Manispaa ya Lindi, Mtaa wa Rutamba alie jinyonga Leo hii Majira ya saa Kum...
Dada Ajinyonga
Nguo iliyotumika kuchukua Uhai wa Mwanahamisi Ismail Mkazi wa Manispaa ya Lindi, Mtaa wa Rutamba alie jinyonga Leo hii Majira ya saa Kumi Jioni Chumbani kwake. 
Dada Ajinyonga
Askari waliofika katika eneo la Tukio wakimtoa marehemu Mwanahamisi Ismail (28) Mkazi wa Mtaa wa Rutamba Manispaa ya Lindi Baada ya Kukutwa kajinyonga Chumbani kwake Leo Mchana. 

Na Mwandishi wetu. Lindi
Mkazi mmoja wa Manispaa ya Lindi katika Mtaa wa rutamba amekutwa kajinyonga chumbani kwake kwa kutumia Nguo.

Shuhuda wa Tukio hilo aliyetambulika kwa jina la Halima Mussa ambaye ameeleza kuwa marehemu kabla ya kukutwa na mauti hayo walikuwa nae uani na wakiongea nae kawaida tu lakini inasstajabisha nini kilimkuta hadi kufikia hatua hiyo ya Kujinyonga na kuchukua uhai wake. Shuhuda huyo alihadithia kuwa aliingia ndani ya Chumba ambacho marehemu anaishi kwa kusudi ya kuongeza maji kwenye Mboga iliyokuwa jikoni lakini alimkuta marehemu akiwa ananing'inia na hivyo aliweza kuwaita majirani nakuja kumnasua kwenye kitanzi hicho lakini walikuwa wamesha chelewa kwani mauti tayari yalikuwa yamesha mkuta bi mwanahamisi Ismail.

Jirani yake na Marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Asha Mohamed ameiambia Lindiyetu.com kuwa Marehemu alikuwa Mgonjwa hadi kufukia kupelekwa kwa Mgonga wa jadi ili kupata tiba, aliongeza ya kuwa anashangaa nini kimetokea kwani Tangu arudi kwa Mganga wa Jadi huyo alikuwa yuko sawa na leo hii wameongea na kawaida na hakukua na tatizo lolote sasa inastajabisha sana tukio hili.

Aisha Marehemu Mwanahamisi Ismail ameacha mtoto Mdogo mmoja.

Dada Ajinyonga
Majirani wakitoa Mwili wa Marehemu Mwanahamisi Ismail tayari kumpeleka Hospitali ya Sokoine kwa ajili ya Vipimo zaidi.... 
Dada Ajinyonga
Polisi walisimamia kikamilifu zoezi hilo la Kupeleka mwili wa Marehemu katika Hospitali ya Mkoa ya Sokoine 
Dada Ajinyonga
Mwili wa Mareehemu Mwanahamisi Ismail ukiwa ndani ya Gari la Polisi tayari kuelekea hospitali. 
Dada Ajinyonga
Majirani na Ndugu wa Karibu wakiwa Tayari kuusindikiza Mwili wa marehemu Mwanahamisi Ismail aliyekutwa kajinyonga Chumbani kwake leo Mnamo saa Kumi jioni. 
Dada Ajinyonga
Safarri Ilianza kuelekea Hospitali 
Dada Ajinyonga
Nyumba aliyokuwa akiishi Marehemu Mwanahamisi Ismail enzi za Uhai wake.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top