Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dk. Charles Msonde.
Watahiniwa watakaojisajili katika kipindi cha kawaida yaani tarehe 01 Januari 2015 hadi 28 Februari 2015 watalipa ada ya Shilingi 50,000/- kwa wanaojisajili mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Shilingi 30,000/- kwa wanaojisajili mtihani wa Maarifa (QT).
Watahiniwa watakaojisajili kwa kuchelewa yaani kuanzia tarehe 01 Machi 2015 hadi tarehe 31 Machi 2015 watalipa ada ya Shilingi 65,000/ kwa Kidato cha Nne na ada ya Shilingi 40,000/- kwa mtihani wa Maarifa (ada pamoja na faini).
Waombaji wote watajisajili kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Baraza la Mitihani: www.necta.go.tz. Kabla ya kujisajili kwenye mtandao waombaji watapaswa kwenda kwenye vituo wanavyokusudia kufanyia mtihani kuchukua namba rejea (Reference Number).
Wakuu wote wa vituo nchini wamekabidhiwa namba rejea na watazigawa kwa watahiniwa tarajali bila malipo.
Aidha waombaji watapaswa pia kulipa ada ya mtihani kwa njia ya Posta au M-Pesa kabla ya kujisajili kwani hakuna mtahiniwa atakayeweza kujisajili bila kulipa ada ya mtihani.
Waombaji wote wazingatie kwamba kipindi cha usajili kitafungwa rasmi tarehe 31 Machi 2015
Imetolewa Na: KATIBU MTENDAJI
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.