Unknown Unknown Author
Title: #SPORTS:: LIGI DARAJA LA TATU:: STAND WORIOUS WAIBANJUA MAGEREZA FC 1 - 0
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kikosi cha Kwanza cha Stand Worious kilichocheza dhidi ya Timu ya Magereza Fc Leo hii Kinachofundishwa na Ibrahim Ibrahim, Katika Ligi D...
kikosi cha Stand Worious
Kikosi cha Kwanza cha Stand Worious kilichocheza dhidi ya Timu ya Magereza Fc Leo hii Kinachofundishwa na Ibrahim Ibrahim, Katika Ligi Daraja la Tatu Mkoa wa Lindi katika Uwanja wa Ilulu
kikosi cha Magereza Fc
Kikosi cha Kwanza cha Magereza Fc kilichocheza dhidi ya Timu ya Stand Worious Leo hii, Katika Ligi Daraja la Tatu Mkoa wa Lindi katika Uwanja wa Ilulu

Na. Mwandishi Wetu, Lindi
Ligi daraja la Tatu Mkoa wa Lindi Imeendelea Leo Hii kwa Kuzikutanisha Timu Mbili za Manispaa ya Lindi, Timu ya Stand Worious Yenye Maskani  yake Stand Kuu ya Lindi na Timu ya Maafande wa Magereza Katika Dimba la Ilulu.

Ikiwa inapoint 2 kabla ya Ushindi wa Leo Timu ya Stand worious iliyokuwa inashika nafasi ya NNE ya Ligi hiyo Imeweza Kukwea nafasi Mbili Juu na Kuifikia Timu Inayoongoza Ligi kwa Kuwa na Point Sawa, Timu ya Marketi Fc zikiwa zote zina Point 5.

Hivyo na Kufanya Mchezo wa Mwisho kutabiriwa kuwa na Upinzani wa aina yake kwani Timu Hizo zitakutana zenyewe kwa zenyewe katika Kukamilisha Ratiba hiyo na Kufanya Timu zote kuwa na Kiu ya Kumaliza Ligi hiyo akiwa Mbabe. Timu ya Magereza Imebakia Mkiani mwa Ligi hiyo Kwa Kujikusanyia Point Moja Tu hadi sasa.

Katika Mchezo wa Leo Timu zilianza kwa Kushambuliana Kwa zamu Japo Pande zote mbili Washambuliaji wake hawakuwa Makini Kumalizia Mashambulizi yaliyokuwa yanafika langoni kwa Mwenzake.

Hadi Timu hizo Zinakwenda Mapumziko Hakuna Aliyeona Lango la Mwenzake. (Stand 0 - 0 Magereza)

Stand Worious wakishangilia Goli
Kipindi cha Pili kilianza kwa Timu zote Kufanya Mabadiliko ya Wachezaji wake. Iliwachukua Dakika Moja tu Timu ya Stand Worious Kuweza kupata Bao la Kuongoza Kupitia kwa Mshambuliaje wake machachali Andrea Kaliati kwa kuweza kufungu goli hilo kwa kutumia makosa ya beki wa Magereza ambaye aliukosa mpira uliopigwa na kumkuta Andrea naye hakufanya Ajizi na kuweza Kumchenga Kipa na Kuweza Kuweka Mpira Wavuni.

Hadi Kipenga cha Mwisho Matokeo yalibakiwa kusomeka ( Stand 1 - 0 Magereza).

Hizi Ni baadhi ya Picha za matukiwa Kiwanjani:;
Kocha wa Magereza akitoa maelekezo
Kocha wa Magereza FC akitoa maelekezo wakati wa Mapumziko

Kocha wa Stand Worious akitoa maelekezo
Kocha wa Stand Worious akitoa maelekezo wakati wa Mapumziko 
Mashabiki wa Mpira wakifuatilia kwa Makini Mchezo huo ambao Stand Worious waliibuka Washindi wa 1-0. 
Heka Heka katika Lango la Magereza Fc....ambayo haikuzaa matunda 
Wachezaji wa Stand Worious wakishangilia mara baada ya Mchezaji Andrea Kufunga Goli la Kwanza dhidi ya Magereza Fc 
Wachezaji wa Stand Worious wakishangilia mara baada ya Mchezaji Andrea Kufunga Goli la Kwanza dhidi ya Magereza Fc  
Mashabiki walifurika Ndani ya Uwanja wa Ilulu kushuhudia Mtanange Huo 
Hii ni moja ya Mchomo Mkali ambao Golikipa wa Magereza aliuokoa......

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top