SHERIA NGOWI AJA NA ZAWADI HII KWA WATANZANIA, ASEMA WAO NDIO WAMEMFANYA AFAHAMIKE KIMATAIFA

Mwanamitindo wa kimataifa kutoka Tanzania, Sheria Ngowi, amewataka watanzania kukaa mkao wa kula kutokana na kuwaandalia bidhaa mbalimbali zenye ubora ambazo ni kutokana na kutambua mchango wao katika kazi zake.
Sheria Ngowi
Amesema kuwa kutokana na kuona umuhimu wa kuwapa watanzania bidhaa zenye ubora mwaka huu anawaandalia bidhaa mbalimbali ziliwepo ngua za watoto, ndala, kaptula na suti za kike.

Akiongea na Kituo kimoja cha redio nchini, amesema kuwa ili kuweza kuwafikia watanzania kiurahisi ameona bora kuwaandalia nguo ambazo wakiwa katika mazingira ya ofisi, nyumbani na hata katika shughuli wanaweza kupata mavazi yake.

“Watanzania ni watu ambao nawapenda sana bila wao leo sijui hata kama ningeweza kufahamika, nataka kila siku mtu ajivunie kuvaa nguo au bidhaa yoyoye ambayo ni kazi ya mkono wangu, akikosa viatu, ndala, kaptula, suti na nguo za shughuli basi hata tai aipate,” alisema Sheria.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post