Unknown Unknown Author
Title: JITIHADA ZA SERIKALI UJENZI WA BARABARA NDUNDU-SOMANGA ZILIMREJESHA MFADHILI, SASA YAMALIZIKA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
MUSSA IYOMBE Katibu wa Wizara ya Ujenzi Nchini Tanzania Akiongea na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa Uzinduzi wa Kipande ...
Ndundu - Somanga
MUSSA IYOMBE Katibu wa Wizara ya Ujenzi Nchini Tanzania Akiongea na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa Uzinduzi wa Kipande cha Bara bara cha Ndundu - Somanga Kilichomalizika kwa Ujenzi wa Kiwango cha Lami

Na. Abdullaziz, Lindi
Jitihada za serikali ya Tanzania kukamilisha mradi wa ujenzi wa barabara ya Ndundu hadi Somanga kwa kutumia fedha za ndani zilisababisha Nchi ya Kuwait kurejea tena na kushirikiana na Serikali kujenga barabara hiyo.

Hayo yameelezwa jana na katibu wa wizara ya ujenzi, Mussa Iyombe wakati wa uzinduzi wa barabara hiyo uliofanyika kijijini Somanga wilaya ya Kilwa mkoani Lindi.

Iyombe alisema nchi ya Kuwait iliposita kuendelea kufadhili ujenzi barabara hiyo yenye urefu wa kimometa 60, serikali iliendelea na ujenzi kwa kutumia fedha za ndani na kusababisha Mfadhili huyo kurejea na kuungana na serikali katika ujenzi huo.

Alisema awali ilikadiriwa ujenzi wa kipande hicho ungegharimu shilingi bilioni 58. Hata hivyo kutokana na ujenzi huo kuchelewa kukamilika, gharama ilipanda na kufikia shilingi bilioni 66 hadi kukamilika.

Iyombe aliwaasa watumiaji wa barabara ikiwamo madereva kuitunza barabara hiyo kwa kuepuka kufanya iharibike na kudumu kwa muda mfupi ikiwamo kupakia na kusafirisha mizigo mikubwa isiyositahili kusafirishwa kwa kutumia barabara.

Kwa upande wao baadhi ya madereva licha ya kuishukuru serikali kwa kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo lakini pia waliiomba kuendelea na jitihada hizo ili kujenga vipande viliyosalia ili kuunganisha na barabara hiyo ikiwamo barabara ya Ruangwa hadi Lindi, Nachingwea hadi Nanganga na Masasi hadi Nachingwea.

Ndundu - Somanga
Kipande Korofi cha Barabara cha Ndundu - Somanga Chakamilika kwa Kiwango cha Lami, Kandarasi anamalizia Mifereji katika Barabara Hiyo 
Ndundu - Somanga

Ndundu - Somanga
MUSSA IYOMBE Katibu wa Wizara ya Ujenzi Nchini Tanzania Akiongea na Waandishi wa Habari wakati wa Ufunguzi wa Barabara ya Ndundu - Somanga Mkoani Lindi.
Ndundu - Somanga
Mhandisi wa Mkoa wa Lindi Eng. Isack Mwanawima akitoa maelezo kwa Waandishi wa habari, katika Ufunguzi wa Kipande cha Barabara cha Ndundu - Somanga, Hapo Jana 
Ndundu - Somanga
Mabasi yakianza Kupita katika Kipande hicho kilichomalizika cha Ndundu - Somanga Mkoani Lindi 
Ndundu - Somanga
Hakika Sasa wakazi wa Kusini wapata faraja katika Umalizikaji wa Kipande hichi kilichokuwa Kikwazo kikubwa katika sekta ya Usafiri mikoa ya Lindi na Mtwara. 
Ndundu - Somanga
Dereva alkizungumza na Waandish wa habari kuhusiana na Umalizikaji wa Kipande hicho cha Ndundu - Somanga, ameipongeza Serikali katika suala hilo. 
Ndundu - Somanga

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top