IRAQ, WATOTO WALEMAVU WANAENDELEA KUTUMIWA KUFANYA MASHAMBULIZI YA KIGAIDI

Ukiukaji wa haki za watoto unaendelea nchini Iraq, ambako watoto walemavu wanaendelea kutumiwa kufanya mashambulizi ya kigaidi, kwa imani kuwa wataweza kupona.BOMUKatika ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini Iraq, wataalam wa haki za binadamu wameelezea pia kwa kina kuhusu kutumia watoto katika biashara ya ngono na kutengeneza picha na filamu za ngono, pamoja na vitendo vingine katili vinavyowalenga watoto wa kike.
Wataalam walioichangia ripoti hiyo wamesema matatizo mengi ya Iraq yalikuwepo hata kabla ya uvamizi wa kundi la kigaidi linalotaka kuweka dola la Uislamu wenye msimamo mkali, ISIL, mnamo mwaka 2014.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post