Unknown Unknown Author
Title: HILI NDILO VAZI LA TAIFA ALILOWAKILISHA NALE BONIFACE MISS UNIVERSE TANZANIA 2014, HUKO MAREKANI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mashindano ya awali (Preliminary show)ya fainali za kumtafuta mrembo wa Miss Universe Kimataifa huko jijini Doral, Miami-Marekani yamefanyi...
Mashindano ya awali (Preliminary show)ya fainali za kumtafuta mrembo wa Miss Universe Kimataifa huko jijini Doral, Miami-Marekani yamefanyika jana tarehe 21 huku jumla ya warembo 88 kutoka nchi tofauti duniani wakipita na mavazi ya Kitaifa(National Costume), ufukweni(Swim Suit) na magauni ya usiku(Evening gown).
Mrembo wa Tanzania, Nale Boniface (pichani) ni mmoja wa washiriki wa mashindano hayo ambapo fainali zake zitahitimishwa jumapili, januari 25 huko Marekani.

Siku chache zikiwa zimebakia kuhitimisha shindano hilo, washiriki wote walipata nafasi ya kuzungumza na kuhojiwa na vyombo mbalimbali vya habari huku wakizungumzia mawazo yao kuhusu fainali hizo.

Shindano hilo la awali liliendeshwa na mrembo wa Miss Universe 2013, Gabriela Isler and Roxanne Vargas. Shindano hili la awali lilikuwa na umuhimu kwa washiriki wote kwani ndipo wanapopatikana 16 bora ambapo watatangazwa siku ya fainali za shindano hilo jumapili ya tarehe 25. Shindano hili ni la 63 kufanyika toka kuanzishwa kwake.

Mshiriki wa Tanzania katika shindano hili alivaa vazi lililobuniwa kutokana na zao la MKONGE. Mkonge ni zao linalo stahimili ambapo linaweza kustawi katika hali ya ukame na nchi zenye uoto usio na rutuba.

Zao hili pia lina magonjwa machache sana ambayo mara nyingi halihitaji dawa yoyote. Pia zao hili linasaidia kuzuia mmomonyoko wa udongo na kupata unyevu wa anga. Zao hili linaweza kupandwa wakati wowote wa mwaka na kuvunwa kwa mwaka mzima.

Zao hili pia haliathiriwi na moto, na ni mazao machache sana katika dunia hii yenye sifa kama hizi. 
Hivyo, vazi la mshiriki wetu wa Tanzania katika fainali za Miss Universe limebuniwa na kutengenezwa kutokana na zao la Mkonge.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top