DIAMOND PLATINUMZ, RAIS JK SIRI NZITO....!


Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK’.
Rais wa Wasafi Classic Baby (WCB), Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK’.

NYUMA ya ukaribu wa Rais wa Wasafi Classic Baby (WCB), Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK’, kuna siri nzito kufuatia mambo mbalimbali yanayojitokeza kati yao kila kukicha, Amani lina cha kukujuza.
Katika kuunga maelezo hayo, inasemekana kwamba mbali na mambo mengine, hivi karibuni Diamond alimpelekea JK tuzo zake tano za kimataifa alizotwaa mwaka 2014 kwa kuwa nyuma yake kulikuwa na sapoti kubwa ya mkuu huyo wa nchi.

UKARIBU MKUBWA Kwa mujibu wa chanzo cha karibu ambacho ni ‘mtu’ wa Diamond, staa huyo amekuwa ‘klozdi’ sana na JK kufuatia mambo yake mengi ya msingi kuyafanya kwa kumshirikisha, kiasi kwamba kuna wakati Diamond hata akikurupuka usiku wa manane kama ana jambo huwa hasiti kumpigia simu mheshimiwa na kuongea kwa muda huku wakicheka weee!
>>Jamii Blog

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post