BABA MZAZI WA MSANII WA NIGERIA YEMI ALADE AFARIKI DUNIA, SOMA ALICHOKISEMA YEMI BAADA YA KIFO HICHO

Yemi Alade
MWIMBAJI maarufu wa kimataifa wa Nigeria, Yemi Alade, amezungumzia kwa mara ya kwanza kifo cha baba yake aliyefariki wiki iliyopita.

Msanii huyo wa kike aliyevuma kwa wimbo wa ‘Johnny’, alitoa kauli yake katika mtandao wa kijamii wa Instagram ambako aliandika: “Mungu ambariki. Mbingu imepata malaika mwenye thamani kubwa,” aliandika katika ukurasa wake wa Instagram akiambatanisha na picha ya baba yake.

baba yake Yemi.

Marehemu baba yake Yemi.


Kuhusu mazishi ya mzazi wake huyo, Yemi alisema maelezo yatatolewa wakati muafaka.“Asanteni sana kwa ujumbe wenu. Mipango ya mazishi itatolewa wakati ukifika,” aliandika staa huyo.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post