Unknown Unknown Author
Title: WAKURUGENZI WATANO (5) NCHINI WASIMAMISHWA KAZI, KISA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na Bakari Issa,Dar es Salaam Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI leo imetangaza kuwasimamisha kazi Wakurugenzi watano (5) huk...
Hawa Ghasia
Na Bakari Issa,Dar es Salaam
Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI leo imetangaza kuwasimamisha kazi Wakurugenzi watano (5) huku wengine wakipewa onyo kali katika utekelezaji wa majukumu yao.

Akithibitisha kusimamishwa kazi kwa Wakurugenzi hao,Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Mh. Hawa Ghasia amesema kwamba Wakurugenzi hao wametenda makosa yanayowaondolea sifa za kuwa Wakurugenzi.

“Makosa yafuatayo ndio yanayopelekea Wakurugenzi hawa kusimamishwa;Kuchelewa kuandaa vifaa vya kupiga kura,kukosa umakini katika kuandaa vifaa hasa karatasi za kupigia kura,kuchelewa kupeleka vifaa kwenye vituo vya kupigia kura,uzembe katika kutekeleza majukumu yao pamoja na kutoa taarifa za kupotosha kuhusu maandalizi ya uchaguzi kuwa yamekamilika huku wakijua kuwa siyo kweli”,alisema Ghasia

Aidha, Mh.Ghasia ameridhishwa na hatua ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kumchukulia hatua mtumishi wake aliyemsingizia Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali na kusema ni jambo baya kutenda kosa na kusingizia watu au ofisi zisizohusika.

Wakurugenzi wanaosimamishwa kazi na kupisha uchunguzi zaidi ni pamoja na

i) Bw.Felix T.Mabula-Halmashauri ya Hanang’ii) Bw.Fortunatus Fwema- Halmashauri ya Mbuluiii) Bi.Isabela D.Chilumba- Halmashauri ya Ulangaiv) Bi.Pendo Malabeja- Halmashauri ya Kwimbav) Bw.William Z.Shimweta-Sumbawanga Manispaa


Pia, Mh.Hawa Ghasia amesema Wakurugenzi wengine watatu(3) wanapewa onyo kali na watakuwa chini ya uangalizi kubaini kama wana udhaifu mwingine ili wachukuliwe hatua zaidi Wakurugenzi hao ni:-

i) Bw.Mohamed A.Maje-Halmashauri ya Romboii) Bw.Hamis Yuna- Halmashauri ya Busegeiii) Bw.Jovin A.Jungu- Halmashauri ya Muheza

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top