MWANASHERIA MKUU JAJI WEREMA AJIUZULU WADHIFA WAKE

Jaji Frederick Werema
Mwanasheria mkuu wa serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia leo, jumanne, Desemba 16, 2014 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu.

Taarifa kutoka Ikulu zimesema katika barua yake kwa Mhe. Rais Kikwete, Jaji Werema amesema kuwa ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya akaunti ya Tegeta Escrow hakueleweka na umechafua hali ya hewa.

Mhe. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post