MANCHESTER UNITED YAIBANJUA STOKE CITY 2-1, OLD TRAFORD

Manchester United
Timu ya kocha Mholanzi, Louis Van Gaal imeshinda mabao 2-1 Uwanja wa Old Trafford dhidi ya Stoke City katika muendelezo wa mechi za Ligi Kuu.Marouane Fellaini aliifungia Manchester United bao la kwanza dakika ya 21 kwa kichwa, kabla ya Steven Nzonzi kuisawazishia Stoke kwa shuti la mbali dakika ya 39 na Juan Mata kuwafungia bao la ushindi wenyeji kwa mpira wa adhabu dakika ya 59.
Manchester United

Manchester United
United usiku wa jana iliwakosa nyota wake majeruhi Wayne Rooney na Angel di Maria, na kwa ushindi huo ni dalili kwamba Van Gaal anaelekea kuanza ‘kupunga upepo’ Old Trafford.
Manchester United

Kikosi cha Manchester United kilikuwa; De Gea, Valencia, Smalling, Rojo, Young, Fellaini, Carrick, Herrera/Fletcher dk86, Mata, Van Persie na Wilson/Falcao dk78.

Stoke City; Begovic, Bardsley, Shawcross, Wilson, Pieters, Cameron, Nzonzi, Ireland/Arnautovic dk82, Krkic, Assaidi/Crouch dk77 na Diouf.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post