Unknown Unknown Author
Title: DIAMOND PLATNUMZ AFUNGUKA KUHUSU SAKATA LA KUZUSHIWA KUWADHALILISHA WASANII WENZAKE MOMBASA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Diamond Platnumz alikuwa nchini Uganda na Kenya katika Ziara yake ya Utoaji wa Burudani katika Nchi Hizo Wiki iliyo pita, Sasa Kumeibu...
Diamond Platnumz
Diamond Platnumz alikuwa nchini Uganda na Kenya katika Ziara yake ya Utoaji wa Burudani katika Nchi Hizo Wiki iliyo pita, Sasa Kumeibuka na Tetesi Kuwa aliweza kuwa Nyanyasa wasanii wenzake wa nchi ya Uganda "Nyota Ndogo na Susumila"

Kutokana na Sakata hilo Kuripotiwa na Chombo kimoja cha habari Diamond Platnumz ameweza Kukanusha Tetesi hizo na Kusema Haya kupitia moja ya Account yake ya Social Networks...
"Nimesikitishwa Sana na habari zilizoandikwa na moja ya chombo cha habari, kuwa eti nliwanyanyasa wasanii wenzangu Nyota ndogo na Susumila, kwa kuwafukuza kwenye VIP lounge na sijui eti niliwazuia wasitumie maji ya chupa hivi inaingia akilini kweli hii!!!?? Ningependa kutumia nafasi hii kuwajulisha mashabiki zangu waliokutana na story hizo kuwa sio za kweli ni zenye lengo la kudhoofisha Mahusiano yetu mazuri ya wasanii Wa Africa mashariki..kama BigEye ya Uganda ilivyowahi kuandika habari za upotoshaji Kati yangu na Jose Chameleone.. Pia Nawasihi @Bongofive ni vyema mtambue Nafasi yenu kwenye jamii kwa sasa, Kuweni makini na baadhi ya habari mnazo post ama kureport kutoka baadhi ya mitandao, zinavunja mahusiano mazuri ya wasanii wa East Africa...kumbukeni kuna watu wana tabia ya kujudge kitu kwa kusoma kichwa cha habari tu pasipo kufuatilia undani wa habari...Yawezakuwa mwaandika kwa nia njema tu, lakini ni vyema muwe mnapata na uhakika kwanza kabla ya kuripoti, hususan story za kutengeneza chuki kama hizi....kufanya hivyo ndiyo mtasaidia kukuza industry yetu ya East Africa..."
Kauli ya Msanii Susumila
Susumila
Susumila

“Hizo story ni za uongo,” amesema msanii huyo. “Sidhani kama Diamond anaweza kufanya hivyo au ana haki ya kufanya hivyo. Kama nimekuwa mistreated labda niwe mistreated na yule mtu amenipatia show, sio Diamond sababu naye ameitwa kwenye show kama mimi,” ameongeza.

“Unajua Mombasa wanapenda vitu vya uongo, hakuna mtu ana complain kuhusu show ilikuwa mbovu ama nini, watu wanatafuta vijisababu vidogo vidogo wanasema sijui nimenyimwa maji. Mimi nilipanda steji nilikuwa na chupa yangu ipo kwa DJ, nikaperformm dancers wangu walipokuwa wameingia wanafanya set yao nikachukua maji nikanywa pale pale kwa DJ kulikuwa na chupa kama kumi za maji hazijafunguliwa. Sijui story ilianzia wapi lakini kufikia kwenye saa tatu, saa nne ilikuwa kwenye blog karibu zote za huku (Mombasa).”

Msikilize zaidi hapo chini.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

  1. Ahsante Mr.Diamond kwa kufunguka. Mijitu bwana aaaaa imekalia umbeya na uzushi tu na hii ndo fahali ya mjinga

    ReplyDelete

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top