BINGWA WA MASUMBWI MOHAMED ALI ALAZWA HOSPITALINI

Mohammed Ali
Aliyekuwa bingwa wa ndondi duniani Mohammed Ali na Mwanawe leila Ali.Bondia huyo mkongwe amelazwa hospitalini akiugua maambukizi ya mapafu.

Aliyekuwa bingwa wa ndondi ulimwenguni Mohammed Ali amelazwa hospitalini baada ya kuugua maambukizi ya mapafu.
Ali ambaye ana umri wa miaka 72 na ambaye ana ugua ugonjwa wa Parkinson anadaiwa kuwa katika hali imara.
Msemaji wake amesema kuwa ugonjwa huo uligunduliwa mapema.


Mohammed Ali
Mohammed Ali wakati wake alipokuwa bingwa wa ndoni duniani.

Hatahivyo hakutoa maelezo zaidi na kutaka haki ya faragha ya familia ya bondia huyo mkwongwe kuheshimiwa.
Ali alipataikana na ugonjwa wa Parkinson mwaka 1984, miaka mitatu baada ya kuustafu katika masumbwi.

Alionekana hadharani katika sherehe moja mnamo mwezi Septemba nyumbani kwake Louisville Marekani wakati wa kutoa tuzo za kibinaadamu za bondia huyo.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post