Unknown Unknown Author
Title: ATELEKEZWA NA WAZAZI WENZA NA KUACHIWA WATOTO 7 HUKU AKIWA NA TATIZO LA MGUU
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
"Mwandishi,umaskini ndio uliosababisha niendelee kutabika na ugonjwa ambao unaweza kutibika na kuwa salama na kufurahia maisha kama ...
Zaria
"Mwandishi,umaskini ndio uliosababisha niendelee kutabika na ugonjwa ambao unaweza kutibika na kuwa salama na kufurahia maisha kama wenzangu" lakini imekuwa kinyume nimeteseka kwa takribani miaka kumi nimekuwa mtu wakusaidiwa hata mlo wasiku moja ila ndiyo mapenzi yake muumba,kutegemea watoto hawa dogo wagonge mawe ambayo yanapatikana mbali kwakubeba kichwani ili tupate mlo nikuishi kwa kudra ya mungu." Hayo nisehemu ya maneno yaliyotokana na mazungumzo baina yangu mimi na Zaria, mkazi wa mtaa wa Mtanda katika halmashauri ya manispaa ya Lindi.

Maelezo ambayo yaliungwa mkono na Noti Gryson Maleko, jirani na msamaria mwema anayemsaidia baadhi ya mahitaji ya kibinadamu na aliyefanikisha kunipata mimi nakuniunganisha na Zaria, ikiwa nimwendelezo wa misaada ya kiutu anayoitoa kwa mama huyo, mama watoto saba ambao wengi wao niwa baba tofauti.Kweli dunia nikubwa na unayoyajua, uliyowahi kuyaona na yale uliyopata kuyasikia ni machache sana katika sayari hii inayoitwa dunia. 

Tena usijione unashida na dhiki kuliko watu wote, utajidanganya na utakuwa unamkufuru mungu kwani kunaviumbe wanapata shida na kuteseka kiasi cha wewe kupata faraja nakujiona hauna shida wala dhiki pindi unapokutana nao. Badala yake utaanza kuwahurumia wao.Ndivyo ilivyo kwa mama huyu ambaye kwa takribani miaka kumi anataabika na kutegemea watoto wadogo kabisa waendeshe nyumba kwa kugonga mawe iliwapate kokoto ambazo wanaziuza ili wapate mlo walau wasiku moja. Mawe ambayo wanayatoa mbali takribani kilo meta 2, usafiri vichwa vyao. 
Zaria
Ilikuwaje hadi amepata tatizo hilo na nitatizo gani hasa linalosababisha aione dunia ni chungu na siyomahali penye fu crewraha? Mama huyo nimarachache sana anamudu kunyanyuka na kutembea walau umbali wa hatua 20 hadi 30. Kinachosababisha ashindwe kutembea na kumsababishia mateso ni maumivu ya mguu ambao umevimba kiasi cha kutisha,ni baada ya kuumwa na mdudu anayedhaniwa kuwa ni nyoka.

Zaria anasema sikumoja akiwa shambani kwa mama yake mdogo aliyemtaja kwa jina la Zaria, ghafla alihisi maumivu makali yaliyoashiria aliumwa na mdudu. Mdudu ambaye baadae ilibainika alikuwa ni nyoka,ni baada ya kufanya utafiti kwa waganga wa jadi wanaoaminika kuwa niwaganga nawajuzi wa masuala ya nyoka katika eneo hilo na ushahidi wa vipimo vya kitaalamu waliambiwa baada ya kupimwa katika hospitali ya Ndanda iliyopo wilaya ya Masasi mkoa wa Mtwara. 

Zaria ameeleza kwamba siku hiyo aliyoumwa na nyoka hakupata usingizi kutokana na maumivu makali.Hali ambayo ilisababisha apelekwe kwa waganga wajadi ambapo mguu huo ulianza kuvimba na kuwa na rangi mweusi. 
Zaria
Hata hivyo juhudi za waganga hao hazikufua dafu bali maumivu yalizidi kuwa makali na mguu kuendelea kuvimba na hivyo kupelekwa katika hospitali ya mkoa wa Lindi (Sokoine) ambako alilazwa kwa muda wa mwezi mmoja na ndipo kwa mara nyingine ilipobainika kuwa aliumwa na nyoka,hata hivyo sumu ilikuwa imekaa kwa muda mrefu mwilini na kusababisha nyama kuanza kuoza. 

Alisema pamoja na kupata matibabu katika hospitali hiyo na kuruhusiwa kurejea nyumbani kwake lakini maumivu yaliendelea kuwa makali na mguu uliendelea kuvimba. Hali ambayo ilisababisha apelekwe katika hospitali ya Ndanda ambako alilazwa kwa muda wa mwezi mmoja na kufanyiwa upasuaji, ambako pia aliambiwa sumu ili chelewa kuondolewa mwilini."kwakweli baada ya kupata matibabu pale Ndanda maumivu yalitulia, niliruhusiwa kurudi nyumbani nikapewa na dawa za kuendelea kutumia na waliniambia niende tena baada ya mwezi mmoja lli wakamalizie matibabu yangu baada ya kuangalia kiwango cha sumu kama ilikuwa imekwisha au bado hata hivyo tangu muda huo sikwenda tena uwezo mdogo" Zaria anaamini kuwa kama angekwenda tena katika hospili hiyo angeweza kupona kutokana na jinsi alivyopata nafuu baada ya kupata matibabu.

"dhiki imesababisha niwe mtumwa na kuwaamini wanaume ambao baadae wameniongezea maumivu kwa kuniongezea mzigo wa watoto ambao sina uwezo wa kuwasomesha,badala yake wameungana namimi mama yao tupate shida hapa duniani inaniuma sana lakini sina jinsi nimeharibikiwa kotekote." 
Mwisho wa maelezo yote Zaria anataka nini kwa jamii na taasisi na mashirika mbalimbali yatayoguswa na tatizo lake? Kama nilivyotangulia kusema katika makala haya ya maisha, kwamba Zaria bado anaimani kuwa ugonjwa alionao unatibika. Hasa kwakuzingatia maelezo ya madaktari wa hospitali ya misheni ya Ndanda ambao wamemthibitishia kuwa tatizo hilo lingekwisha kwani mfupa haujaathirika. Ambapo bado anaimani kwamba akifanikiwa kwenda katika hospitali hiyo anaweza kutibiwa na kupona.

Lakini pamoja na masahibu aliyonayo mama huyo na kutokana na shida alizonazo zimesababisha aamini kila aliyembele yake anaweza kumsaidia. Ni nafasi ambayo watu wasionahuruma wenye roho yakutu walizokopeshwa na shetani(Iblisi) kutumia nafasi hiyo kumlaghai na kuhaidi kumsaidia iwapo atafanyanao mapenzi. Hali iliyosababisha wamzalishe na kumkimbia pindi wanapogundua anaujauzito.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top