ALICHOKISEMA SHEDDY CLEVER JUU YA KUTOANDIKWA KWENYE VIDEO YA WIMBO WA "NITAMPATA WAPI" WA DIAMOND PLATNUMZ

Producer wa hits mbili za Diamond Platnumz ‘Number One’ na ‘Ntampata Wapi’ alionekana kufurahia mafanikio ya Diamond kwenye tuzo za Channel O, lakini kitu kimoja hakijakaa sawa moyoni mwake.
Sheddy Clever
Sheddy amesema ameshangazwa baada ya kutoona jina lake likiandikwa kwenye video ya ‘Ntampata Wapi’.

“Biashara kweli ni matangazo na nilitakiwa niandikwe kweli kwenye ile video, lakini sasa kwa sababu imeshapita na vitu vingi vimeshatokea na ukiangalia kwenye video international wanafanya hivyo ila mpaka sasa hivi najaribu kujiuliza sijapata jibu kamili kwanini wanafanya hivyo,” Sheddy ameiambia E-News ya EATV.

“Ukiangalia video za West Africa za akina Davido, Wizkid wengi producer wa audio wanakuwa hawaandikwi kwenye video. Sasa sijui wanafuta ule mfumo wa wenzetu, sifahamu.” Sheddy aliongeza

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post