ZARI THE BOSS LADY AFUNGUKA JUU YA TETESI ZA KUTOKA NA DIAMOND PLATNUMZ, BAADA YA PICHA ZAO ZA UTATA KUENEA MITANDAONI


Mfanyabiashara na mwimbaji mrembo wa Uganda, Zari the Boss Lady na Diamond Platnumz waliingia kwenye headlines weekend iliyopita baada ya picha zao wakiwa kwenye faragha kama wapenzi kuzua maswali mengi kwenye mitandao ya kijamii.
Hata Hivyo Zari hakuchukua muda mrefu na kuamua kutumia Instagram kufumbua fumbo hilo kwa kuweka wazi kuwa ameshirikiana na Diamond katika wimbo wake mpya.
Zari ameuambia mtandao wa Big Eye wa Uganda kuwa picha zilizosambaa ni sehemu ya video shoot ya wimbo aliofanya na hit maker wa Number 1.
Wimbo huo unatarajiwa kutoka December 18 wakati wa party ya Zari ‘All white Ciroc party’ itakayofanyika kwenye Club Guvnor nchini Uganda.
Kitu ambacho watu wengi walikuwa hawafahamu ni kuwa , Zari ni muimbaji lakini alikuwa ameweka pembeni muziki kwa muda, na sasa ameamua kurejea.
Tazama video ya moja ya nyimbo alizowahi kutoa.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post