Unknown Unknown Author
Title: TIMU YA POLISI MOROGORO YABARIKIWA KUWA TIMU PEKEE ITAKAYOWAKILISHA JESHI HILO NCHINI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Jeshi la Polisi nchini limeipitisha timu ya Polisi Morogoro kuwa timu pekee ya jeshi hilo huku likitoa agizo kwa wakuu wa Polisi wa mikoa...
timu ya Polisi Morogoro
Jeshi la Polisi nchini limeipitisha timu ya Polisi Morogoro kuwa timu pekee ya jeshi hilo huku likitoa agizo kwa wakuu wa Polisi wa mikoa kuziuza ama kuzigawa timu za soka za mikoa hiyo kwa wananchi ili kutekeleza agizo la shirikisho la soka duniani FIFA ambalo linakataza taasisi moja kuwa na zaidi ya timu moja.

Afisa michezo wa jeshi la polisi SSP Jonas Mahanga amesema wanaliafiki agizo hilo na kwa sasa wanaamini timu nyingine za Polisi za mikoa zitarejeshwa mikononi mwa wananchi na kuitwa majina mengine hali ambayo amesisitiza itakuwa na chachu ya kulete ushindani mkubwa.

Amesema agizo hilo la FIFA limelisaidia jeshi la Polisi nchini kupunguza mzigo wa kuzihudumia timu nyingi kwa wakati mmoja pasi na mafanikio yoyote, hivyo wanaamini timu ya Polisi Mororogo inayoshiriki ligi kuu kwa sasa ndio itakua timu ya jeshi hilo kwa nchi nzima.

Hitimisho hilo la jeshi la Polisi la kuafiki kubaki na timu ya Polisi Morogoro na kuifanya kuwa timu ya jeshi kwa nchi nzima kunamaanisha timu nyingine za jeshi hilo ambazo zinashiriki ligi daraja la kwanza na la pili kama Polisi Mara, Polisi Dodoma, Polisi Dar es salaam pamoja na Polisi Tabora zinakufa kwa kupigwa mnada ama kuzawadiwa kwa wananchi wa mikoa husika.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top