Unknown Unknown Author
Title: SERIKALI YAWASISITIZA WANANCHI WA MKOA WA TABORA KUUTUNZA MTI ULIO ANGUKA NA KUSIMAMA TENA, HABARI KAMILI HII HAPA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Tarehe 15 October huko mkoani Tabora, mti uliokuwa umeanguka miaka mitatu iliyopita ulisimama ghafla na kwa sauti kubwa ya mrindimo.  ...
Tarehe 15 October huko mkoani Tabora, mti uliokuwa umeanguka miaka mitatu iliyopita ulisimama ghafla na kwa sauti kubwa ya mrindimo. 
Mti wa maajabu - Tabora

Wananchi walikusanyika na wanaendelea kukusanyika kila mmoja akitaka kuchukua angalau gome la mti huo kwa ajili ya dawa ama kumbukumbu. Tukio hili la ajabu ambalo limestaajabisha wengi limekaa kwenye headline tena ambapo viongozi wa Serikali wamezungumzia hilo huku wananchi wakisisitizwa kuutunza. 

Katibu tawala wa Wilaya ya Uyuwi amesema; “…kwa mazingira tunayoyaona hapa tukio ni kweli limetokea sasa ni kwa nguvu zipi kwa uwezo wa Mungu au nguvu za giza hili nadhani kwa sasa litakuwa hatuwezi kulitolea taarifa ,lakini cha msingi eneo hili tulitunze kwa matumizi ya kumbumbuku ya vizazi vyetu na pamoja na wengine watakaotoka nje ya eneo hili, ambao watataka kuja kuona maajabu ya Mwenyezi Mungu tofauti na kule Mfuto ulipoinuka tu siku ya pili yake tukakuta kila kitu hakuna, kwa hiyo nilikuwa napenda niwapongeze Wanakijiji kwa kulinda Mti huu…” 

Shuhuda wa kwanza kuzungumzia tukio hilo amesema; “… Haya magome ya mzizi yakichimbwa, yakisagwa mtoto akiwa anaumwa Degedege wakimvutisha ile hali ya mchango inashuka hata kama unaumwa kipanda uso, hata kama unaumwa kichwa cha kawaida…”.

Mwanakijiji mwingine amesema; “…Huu Mti kama mbwa wako sio mkali unachimba mizizi unakoboa magome unatwanga ule unga wake unamnusisha kwenye pua anakuwa mkali sana…" 

Mtu mwingine amesema; “Kama kuna Mtu ambaye pengine kashaishiwa pengine fahamu wanajaribu kumuwekea puani na mara anapiga chafya…” 

Haya ndio maajabu ya Tanzania. Bado nina maswali mengi but sijui majibu ntapata wapi? How did this happen?

BOFYA PLAY KUSIKILIZA MAHOJIANO HAYO:

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top