Unknown Unknown Author
Title: KAMA HUKUPATA KUSIKILIZA RIPOTI YA PAC KUHUSU TEGETA ESCROW HII HAPA, BOFYA USIKILIZE
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Katika kikao cha Bunge kilichokaa leo Novemba 26 Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe na Makamu wake Deo Filikunjombe waliwasilisha Ripoti ya ...
Katika kikao cha Bunge kilichokaa leo Novemba 26 Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe na Makamu wake Deo Filikunjombe waliwasilisha Ripoti ya ishu ya Escrow ambapo kama hukupata kusikiliza wakati Ripoti hiyo ikiwasilishwa hii ni sehemu ya uwasilishwaji wa Ripoti hiyo.
Zitto Kabwe
Mh. Zitto Kabwe akiwasilisha Ripoti ya PAC leo Bungeni Dodoma

“…Katika fedha ambazo zimelipwa kwa watu binafsi katika Benki hizi yapo majina ya viongoozi wa kisiasa, viongozi wa madhehebu ya dini, Majaji na watumishi wengine wa Serikali..“– Zitto Kabwe.

“… Kamati imependekeza kuwa uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali utenguliwe mara moja na kisha afikishwe Mahakamani kwa matumizi mabaya ya Ofisi yaliyopelekea Serikali kupoteza mabilioni ya fedha za umma…“– Deo Filikunjombe.

"Kwa upande wa Waziri Mkuu kuhusiana na suala hili baada ya kupitia vielezo vilivyomo kwenye ripoti ya CAG kamati imejiridhisha pasipo mashaka kuwa Waziri Mkuu alikuwa ana taarifa zote kuhusiana na mchakato mzima wa kuchota fedha kwenye akaunti ya Escrow, ushahidi ulioletwa mbele ya kamati za ofisi ya CAGulionyesha kuwa Waziri Mkuu alikuwa akipata taarifa juu ya jambo hili na kamati imethibitishwa kuona kuwa Waziri Mkuu hakuchukua hatua yoyote kuzuia mhamala huu usifanyike…" – Deo Filikunjombe.

"Kamati kwa kuzingatia kielelezo namba 22 inathibitisha kwamba bila shaka Waziri Mkuu alikuwa analijua jambo hili vizuri sana na kwamba aliridhia mhamala huu usifanyike, ndio maana katika maelezo yake ya Bungeni mara kadhaa Waziri Mkuu alilithibitishia Bunge kuwa fedha za ESCROW hazikuwa fedha za umma…”– Deo Filikunjombe.

Kumsikiliza Zitto Kabwe akiwasilisha Ripoti hiyo, bonyeza play hapa.
Msikilize Hapa Filikunjombe akimalizia Ripoti hiyo, Bofya Play

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top