Unknown Unknown Author
Title: OLD TRAFFORD: MAN UNITED YASHINDA, ROONEY KADI NYEKUNDU, KINDA McNAIR IMARA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Wakicheza kwao Old Trafford, Manchester United wameifunga West Ham Bao 2-1 katika Mechi ya Ligi Kuu England na kukwea hadi Nafasi ya 7 laki...
Wakicheza kwao Old Trafford, Manchester United wameifunga West Ham Bao 2-1 katika Mechi ya Ligi Kuu England na kukwea hadi Nafasi ya 7 lakini watamkosa Nahodha wao Wayne Rooney kwa Mechi 3 zijazo baada ya kutwangwa Kadi Nyekundu.
man united win over west ham united
Hadi Mapumziko Man United walikuwa mbele kwa Bao 2-1 kwa  Bao za Nahodha Wayne Rooney, ambae sasa ametimiza Miaka 10 akiwa Old Trafford, baada kuunganisha pande safi la Rafael katika Dakika ya 5 na Robin van Persie kupiga Bao la Pili katika Dakika ya 22 baada ya kazi njema ya Ander Herrera na Radamel Falcao.
man united win over west ham united
Goli alilofunga Wayne Rooney dakika ya 5 yamchezo katika kipindi cha Kwanza.
man united win over west ham united
Goli alilofunga Robin Van Persie Mnamo dakika ya 22 ya Mchezo katika kipindi cha Kwanza

West Ham walifunga Goli lao baada ya kutokea kizaazaa kufuatia Kona na Diafra Salho kukwamisha Mpira wavuni katika Dakika ya 37.

man united win over west ham united
Dakika ya 54 Man United walibakia Mtu 10 baada ya Refa Lee Mason kumpa Kadi Nyekundu Nahodha Wayne Rooney kwa madai amemchezea Rafu mbaya Stewart Downing.
man united win over west ham united
Hii inamaanisha Rooney atazikosa Mechi 3 za Timu yake dhidi ya Everton,WBA na Chelsea.

Tukio hilo liliwafanya Man United wamtoe Straika Falcao na kumwingiza Kiungo Darren Fletcher.
man united win over west ham united
Katika Mechi hii, Man United walimchezesha Kinda wa Miaka 19 kutoka Timu ya Rizevu, Paddy McNair kama Sentahafu akishirikiana na Marcos Rojos na Kijana huyo alisimama imara.
man united win over west ham united
VIKOSI: MAN UNITED: De Gea, Rafael, McNair, Rojo, Shaw, Blind, Herrera, Di Maria, Rooney, van Persie, Falcao

Akiba: Lindegaard, Thorpe, Fletcher, A Pereira, Valencia, Mata, Januzaj.

WEST HAM: Adrian, Reid, Cresswell, Tomkins, Downing, Sakho, Demel, Amalfitano, Poyet, Song, Valencia

Akiba: Jaaskelainen, Nolan, Zarate, Vaz Te, Jenkinson, Collins, Cole

REFA: Lee Mason

MATOKEO: **Saa za Bongo ***Jumamosi Septemba 27

Liverpool 1 Everton 1
Chelsea 3 Aston Villa 0
Crystal Palace 2 Leicester 0
Hull 2 Man City 4
Man United 2 West Ham 1
Southampton 2 QPR 1
Sunderland 0 Swansea 0
1930 Arsenal v Tottenham

BPL-LIGI KUU ENGLAND
RATIBA: **Saa za Bongo** Jumapili Septemba 28

1800 West Brom v Burnley
Jumatatu Septemba 29
2200 Stoke v Newcastle

LIGI KUU ENGLAND::MSIMAMO
NA
TIMU
P
GD
PTS
1
Chelsea
6
12
16
2
Southampton
6
7
13
3
Man City
6
5
11
4
Swansea
6
2
10
5
Aston Villa
6
-3
10
6
Arsenal
5
4
9
7
Man United
6
2
8
8
Crystal Palace
6
0
8
9
Leicester
6
-1
8
10
Tottenham
5
1
7
11
West Ham
6
0
7
12
Liverpool
6
-1
7
13
Everton
6
-2
6
14
Hull
6
-2
6
15
Sunderland
6
-1
5
16
Stoke
5
-1
5
17
West Brom
5
-4
5
18
QPR
6
-9
4
19
Burnley
5
-3
3
20
Newcastle
5
-6
3
Source:: Soka In Bongo

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top