DIAMOND ATWAA TUZO NYINGINE YA MWAKA .... SOMA HAPA


diamond platnumz
Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz'.
STAA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' ametwaa tuzo nyingine ya Afro-Australia Music and Movie Awards (AAMMA) 2014 kutoka Australia ya Collabo Bora ya Mwaka kupitia nyimbo aliyoshirikishwa na Desert Eagle iitwayo Everyday. Kupitia akaunti yake ya Instagram, Diamond aliyeko nchini Nairobi amewajulisha mashabiki wake kuhusu tuzo hiyo kwa kuandika hivi:
diamondplatnumz ::Ningependa niwajulishe kuwa kijana wenu nimepata tunzo nyingine toka Australia ya Collabo bora ya Mwaka toka kwenye tunzo za #AAMMA_Awards kupitia nyimbo niliyoshirikishwa na Desert Eagle iitwayo #EVERYDAY..... (jus wanted to inform you that, your favourite artist @Diamondplatnunz won another award from Australia on #AAMMA_Awards as best Collaboration song of the Year..)
tuzo
Tuzo waliyopata Dezert Eagle na Diamond Platnumz.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post