TEMBELEA BANDA LA VETA UJIFUNZE VITU VINGI HASA KITEKNOLOJIA NDANI YA VIWANJA VYA NANE NANE - NGONGO, LINDI

Ukifika Viwanja vya Maonyesho ya Nane nane Utaliona Banda Hili na hapa Ndipo Utajifunza Huduma Mbalimbali zinazotolewa na Chuo cha Ufundi Stadi VETA
 
Mkufunzi wa Chuo cha VETA akionesha jinsi ya Kifaa Rahisi cha Kutengenezea Marembo ya Miguu ya Meza au viti kisichotumia Umeme na Ni Rahisi ukitumia naa pia Kukitengeneza na Pia kutoa Kitu bora na kizuri kabisa.
Mambo ya Maakuli hawapo Nyuma Utapata maelezo jinsi gani ya Kuweza kutaarisha Vyakula Tofauti na kupamba chakula kiwe na mvuto kwa mlaji kabla hajakila.
Hapa utaweza Kuona Jinsi Mashine ya Gari inavyofanya kazi kwa Uwazi zaidi hakika Wameweza Elimu yakutosha inatolewa Katika Mabanda haya ya VETA.
Elimu ya ICT nayo inapatikana Ndani ya Banda la VETA
Mtaalamu wa Mambo ya Udongo huyo dah wanawake hakika wanaweza Mdada anatoa maelezo jinsi ya kuweza kuujua udongo gani unafaa kutumika katika kuaandaa Matofali ya kisasa. Ndani ya Banda hilo la VETA
Mambo ya Kimaabara nayo yapo ndani ya Maonesho hayo ya Nane Nane ambayo kwa Mwaka huu yanafanyika Mkoani Hapa Lindi Kitaifa

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post