Unknown Unknown Author
Title: MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA NCHINI (NHIF) UMEWAHIMIZA WANANCHI KUTEMBELEA BANDA LAO KATIKA VIWANJA VYA MAONESHO YA NANE NANE - NGONGO, LINDI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya linalotoa huduma na ushauri katika viwanja vya Nane nane Lindi Mkurugenzi wa masoko na Ut...
Banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya linalotoa huduma na ushauri katika viwanja vya Nane nane Lindi

Mkurugenzi wa masoko na Utafiti NHIF, Raphael Mwamoto akiwa katika Picha ya Pamoja na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Titus Kamani(MB) pamoja Naibu waziri wa kilimo na ushirika, Mhe Godfrey Zambi na Mbunge wa Jimbo la Mtwara mjini, Hasnein Murji mara baada ya ufunguzi wa maonesho ya nane nane mkoani Lindi.

Katibu Msaidizi wa CCM wilaya ya Lindi vijijini, Bw Ngatiche akipima afya yake katika banda la NHIF alipotembelea banda hilo katika viwanja vya nanenane Ngongo.
Naibu waziri wa kilimo na chakula ,Godfrey Zambi akipokea maalezo mbalimbali kuhusiana na NHIF Toka kwa meneja wa mkoa wa Lindi Bi Fortunata Kullaya huku Mkurugenzi wa masoko Bw Raphae mwamoto akisikiliza kwa umakini kuhusiana na Chf inavyofanya vizuri wilayani Nachingwea.
Na..Abdulaziz...-LINDIMfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini (NHIF), umewahimiza wakazi wa mikoa ya Lindi na Mtwara kutembelea banda la mfuko huo kwa ajili ya kupima afya zao kwenye maonyesho ya wakulima 'Nanenane'.

Wito huo umetolewa na Naibu waziri waziri wa kilimo,chakula na Ushirika,ZAMBI Mara baada ya kukagua banda la la mfuko huo katika viwanja vya Ngongo mjini Lindi yanayofanyika kitaifa mkoani humo mwaka huu.

Akiongea na waaandhishi wa habari,Naibu waziri huyo alieleza kuridhishwa kwake na huduma zinazotolewa na mfuko huo hususani mfuko wa Afya jamii (CHF) Ambao kwa aslimia kubwa umeleta tija na kupunguza gharama kwa wateja wake hususan Vijijini.
"Waandishi nawaomba muendelee kuutangaza mfuko wa CHF kwa kuwa mekuwa mkombozi kwa mwananchi mwenye kipato cha chini Ni dhamira ya Serikali kusaidia huduma hii ndio maana michango inayochangiwa jamiii kwa kaya, Serikali nayo hutoa kiasi kama kilichongawiwa ili kuongeza ufanisi wa dawa katika zahanati na vituo vya afya"  Alimalizia Zambi
Akitoa taarifa ya mfuko huo,Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa NHIF, Raphael Mwamoto, alisema hiyo ni fursa kwa wanachama na wasio wanachama wa mfuko huo kujua afya zao ikiwemo kuonana na wataalamu wa huduma za afya kwa ushauri na Tiba bila malipo na huduma zinazotolewa ni kwa kila mmoja si kwa wanachama pekee.

Mfuko unaamini kuwa ni rahisi kudhibiti magonjwa baada ya vipimo kuliko kusubiri kutibu ugonjwa ulioenea mwilini Na ndio maana NHIF Ipo kwa ajili ya jamiii tumejipanga kupima magonjwa mbalimbali ikiwemo vipimo vya kiwango cha sukari mwilini, shinikizo la damu, saratani ya matiti, uzito na urefu, kisha kutoa ushauri wa kitaalam kwa watakaopimwa.
"NHIF Ipo katika maonesho haya hadi siku ya mwisho unaweza fika kujua huduma tunazozitoa ikiwemo kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii na pia tuna madaktari waliobobea kuhakikisha kila anaefika katika banda letu anapata huduma bora"Alimalizia Mwamoto
Maonyesho ya Nanenane yanafanyika Kitaifa Mkoani Lindi katika viwanja vya Ngongo Maonesho yalifunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dr Ally Mohamed Shein

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top