SABBY WA BONGO MUVI: RUSHWA YA NGONO BONGO MUVI IMENITESA

Msanii wa filamu, Salma Omary ‘Sabby’ ameamua kufunguka kuwa ameteswa sana na rushwa ya ngono aliyokuwa akikutana nayo pindi alipokuwa akifurukuta kutoka kisanii.
SABBY
Msanii wa filamu, Salma Omary ‘Sabby’ akipozi.
Akizungumza na Ijumaa Sabby alisema, tatizo hilo la rushwa anaweza kuwa miongoni mwa wasanii waliosumbuliwa sana wakati kuna baadhi walipokuwa wakitolewa nje, walikuwa wanajenga bifu naye na wengine kumtishia kumharibia.
“Mimi kitu ambacho kinaniumiza sana mpaka leo ni jinsi wanawake tunavyodhalilishwa kila siku, naumia mno nimepita katika tabu nyingi mpaka nafikia hapa leo, ila namshukuru Mungu siku zote,” alisema Sabby ambaye ameng’ara kwenye filamu kama vile Siri ya Gining, Hard Price, Moto wa Radi, Dr. Ray na nyinginezo.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post