STEPHEN KESHI AJIUZULU KAMA KOCHA WA NIGERIA {SUPER EAGLES}

Kocha wa Nigeria, Stephen Keshi amejiuzulu kama kocha wa timu hiyo ya Naija baada ya kuondolewa jana kwenye kombe la dunia, FIFA imesema.
Stephen Keshi
Shirikisho la soka la Nigeria bado halijathibitisha kujiuzulu kwake japo ana maswali mengi ya kujibu baada ya timu yake kufungwa 2-0 na Ufaransa Jumatatu hii. FIFA.com imenukuu tweet ya Keshi, japo mapema wakati wa shindano hilo maafisa wa Nigeria walisema hayupo kwenye mtandao huo.

“Friends, it has been a good run and I have enjoyed every moment. It’s been an honour coaching the Super Eagles. It is however time to bow out,” ilisema tweet hiyo.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post