RAIS WA ARGENTINA CRISTINA FERNANDEZ DE KIRCHNER AMPA MAPOKEZI YA HESHIMA MCHEZAJI LIONEL MESSI, CHEKI HAPA

rais wa argentina akiwapongeza wachezaji
Rais wa Argentina Cristina Fernandez de Kirchner (kulia) akimsalimia mchezaji Lionel Messi mara baada ya kuwapokea leo baada ya kurudi nchini kwao.

Mchezaji wa Argentina Lionel Messi leo Julai 13, 2014 amepokelewa nchini kwao na Rais Cristina Fernandez de Kirchner mara baada ya kushinda zawadi ya Mpira wa Dhahabu iliyotokana na kuwa mchezaji bowa katika mashindano ya Kombe la Dunia yaliyomalizika jana nchini Brazili. Mshabiki wengi wa soka wamempongeza sana mchezaji huyo kwa jinsi alivyocheza japo timu yake haikuweza kuwashinda Wajerumani.
rais wa argentina akiwapongeza wachezaji
Rais wa Argentina akimpa pongenzi meneja wa timu yao Alejandro Sabella.Pembeni ni mchezaji Lionel Messi.
rais wa argentina akiwapongeza wachezaji
Viongozi wa nchi ya Argentina wakifurahia jambo mapema leo mara baada ya kurudi nchini kwao.
kipa wa ujerumani akiwa na messi
Wachezaji:: Messi akiwa ameshikilia medali yake ya dhahabu baada ya kuibuka mchezaji bora katika mashindano ya kombe la dunia 2014 yaliyomalizika jana nchini Brazili na Kipa Bora wa Mashindano hayo wa timu ya Ujerumani ambaye timu yake aliiwezesha kuibuka washindi.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post