Unknown Unknown Author
Title: SIKU YA MSANII YAZINDULIWA RASMI NCHINI TANZANIA, KUATHIMISHWA OCTOBA 25 KILA MWAKA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Haak Neel Production ...
Siku ya Msanii
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Haak Neel Production (T) Limited Bw. Emmanuel Mahendeka wakati wa hafla ya uzinduzi wa siku ya Msanii itakayoadhimishwa tarehe 25 Oktoba,Siku ya Msanii inaratibiwa kwa ushirikiano baina ya Baraza la Sanaa la Taifa BASATA na Kampuni hii ya Haak Neel Production. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga na Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA Bw. Godfrey Mungereza.
Siku ya Msanii
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga akiongea na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa siku ya Msanii itakayoadhimishwa tarehe 25 Oktoba, Hafla hii imefanyika mwishoni mwa wiki hii katika Hotel ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam.
Siku ya Msanii
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Haak Neel Production (T) Limited Bw. Emmanuel Mahendeka wakati wa hafla ya uzinduzi wa siku ya Msanii,mapema wikiendi hii, jijini, katikati ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko na Kaimu Katibu wa BASATA Bw. Godfrey Lubejo Mungereza.
Siku ya Msanii
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (katikati) akishiriki kuwakumbuka Wasanii waliotangulia mbeleza za haki, kabla ya kuendelea na hafla ya uzinduzi wa Siku ya Msaanii itakayokuwa inaadhimishwa tarehe 25 Oktoba kila mwaka.Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Bibi. Sihaba Nkinga, Mkurugenzi Mkuu wa Haak Neel Production Bw. Emmanuel Mahendeka na Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA Bw. Godfrey Mungereza.
Siku ya Msanii
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) akielezea kwa ufupi histori ya Siku ya Msanii wakati wa hafla ya uzinduzi wa Siku hiyo itakayokuwa ikiadhimishwa tarehe 25 Oktoba kila mwaka.
Siku ya Msanii
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Haak Neel Production (T) Ltd Bw. Emmanuel Mahendeka akizungumza na wadau wa sanaa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Siku ya Msaanii iliyozinduliwa mapema wikiendi hii jijini Dar es Salaam.
Siku ya Msanii
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akipiga Gitaa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Siku ya Msanii itakayokuwa ikiadhimishwa tarehe 25 Oktoba kila mwaka
Siku ya Msanii
Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni wa India hapa nchini Bibi. Chitra Suresh (wapili kutoka kulia) akifuatilia baadhi ya kazi za wasanii wakati wa hafla ya uzinduzi wa Siku ya Msanii mapema wikiendi hii jijini Dar es Salaam.
Siku ya Msanii
Mwanamitindo mkongwe Asiah Idarius wa kwanza akiwa na baadhi ya wanamitindo wake wakati wa hafla ya uzinduzi wa hafla Siku ya Msanii mapema wikiendi hii.
Siku ya Msanii
Wasanii wa Kikundi cha Ngoma kutoka Dodoma wakitumbuiza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Siku ya Msaani mapema wikiendi hii jijini Dar es Salaam.
Siku ya Msanii
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akipokea zawadi ya gauni kutoka kwa mbunifu wa mavazi na Mwanamitindo Asiah Idarius(katikati) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Siku ya Msaani mapema wikiendi hii jijini Dar es Salaam.
Siku ya Msanii
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (mwenye koti jeupe) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi Sihaba Nkinga wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Sanaa wakati wa hafla uzinduzi wa Siku ya Msanii iliyofanyika mapema wikiendi hii jijini Dar es Salaam.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top