Unknown Unknown Author
Title: MJUE JUST FONTAINE NA REKODI YAKE YA MAGOLI KOMBE LA DUNIA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Pengine huyu ndiye mshambuliaji bora zaidi kuwahi kutokea katika historia ya kombe la dunia tangu kuanzishwa kwake mwaka 1930 huko Montev...
Fontaine
Pengine huyu ndiye mshambuliaji bora zaidi kuwahi kutokea katika historia ya kombe la dunia tangu kuanzishwa kwake mwaka 1930 huko Montevideo Uruguay.Achana na Ronaldo de Lima aliyetumia michuano minne ya kombe la dunia kufunga magoli 15 ama Gerd Muller aliyehitaji michuano miwili kufunga goli 14 lakini habari ni tofauti kabisa kwa huyu mfaransa Just Fontaine ambaye alihitaji mechi 6 tuu kufunga mabao 13 katika michuano iliyofanyika nchini Sweden mwaka 1958.

Je,Fontaine ametokea wapi?
Kama ilivyo kwa nyota wengi wa kifaransa Fontaine ni mzaliwa wa Marrakech nchini Morocco toka kwa mama raia wa Hispania na baba mfaransa mwenye asili ya morocco

Atua vipi Ufaransa?
Baada ya kufanya vizuri akiwa na klabu ya USM Casablanca 1950-53 atua Nice na kuifungia mabao 44 ndani ya misimu mitatu na kuvivutia vilabu vingi lakini ilikuwa ni Stade de Reims iliyobahatika kuipata saini yake 1956 na kutengeneza partnership kali na Raymond kopa aliyehamia Real Madrid mwaka 1958.Akiwa na Reims Fontaine alifunga jumla ya mabao 121 katika misimu 6 huku jumla akiwa kafunga mabao 165 katika michezo 200.
Fontaine
Timu ya taifa
Aitwaa timu ya taifa tarehe 17 disemba 1953 na kufunga hat-trick katika mchezo wake wa kwanza ambapo Ufaransa ilishinda 8-0 dhidi ya vibonde Luxembourg.

Kombe la dunia
Aenda kombe la dunia Sweden akiwa na rekodi ya bao 1 ndani ya miezi 58 ya kuwa nje ya kikosi kutokana na majeruhi.

Afungua akaunti ya mabao kwa kufunga hat-trick dhidi ya timu ya Uruguay katika mchezo ulioisha kwa Ufaransa kushinda mchezo huo kwa mabao 7-3.Afunga tena bao 2 dhidi ya Yugoslavia katika mchezo ambao Ufaransa ilishinda 3-2 huku katika mchezo wa tatu akifunga 1 na kutengeneza 1 katika mchezo ulioishA kwa ufaransa kushinda kwa bao 2-1 dhidi ya Scotland na kutinga robo fainali.

Katika mcheZo Wa robo fainali dhidi ya Ireland ya kaskazini iliyokuwa dhaifu licha ya kutinga hatua hiyo Ufaransa ilishinda mabao 4-0 huku Fontaine akifunga mabao mawili.

Katika hatua ya nusu fainali Ufaransa ilikutana na Brazil iliyokuwa na nyota kama Pele,Vava,Didi,Mario Zagallo,Garrincha,Nirton Santos ambapo Ufaransa ililala kwa mabao 5-2 huku Fontaine akifunga bao 1 dakika ya 7 ya mchezo.

Katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu dhidi ya Ujerumani magharibi Fontaine afunga bao NNE katika mchezo ambao Ufaransa ilishinda 6-3 na kukipatia nafasi ya 3 kikosi cha kocha Paul Nicolas na kuvunja rekodi ya mabao 11 iliyowekwa na Sandor Kosciss wa Hungary 1954 katika kombe la dunia.

Mpaka mwisho wa michuano hiyo Fontaine alikuwa na jumla ya mabao 13 katika michezo 6 pekee lakini kwa bahati mbaya hakurudi na chochote nyumbani kwani wakati huo hakukuwa na zawadi ya kiatu cha dhahabu kwa mfungaji bora.Atangaza kustaafu baada ya misimu miwili yaani mwaka 1960 akiwa na miaka 28 na miezi 11 kutokana na majeruhi na kuweka rekodi ya mabao 30 katika michezo 21 ya timu ya taifa 1967 Apewa kibarua cha kuinoa timu ya taifa na kutoswa baada ya michezo miwili pekee kutokana na yote kuambulia vipigo
Fontaine
MAFANIKIO
1958-mfungaji bora kombe la dunia
1958/59-Mfungaji bora ligi ya mabingwa Ulaya 
1957-60 akiibuka mfungaji bora division 1(ligi 1) mara mbili

Anazungumziaje michuano ya siku hizi?
Fontaine anaona michuano ya siku hizi kuwa ni rahisi kidogo tofauti na ile ya zama zao kwani licha ya kucheza katika viwanja vibovu anasema hata aina ya mipira ilikuwa ni changamoto nyingine kwani licha ya uzito wake pia haikuwa bora kama ilivyo sasa.Anasema zama zao waamuzi hawakuwa na tabia ya kuwalinda washambuliaji kama ilivyo leo anakumbuka pia karibu mashindano yote alicheza kwa kutumia viatu vya kuazima kutokana na uhaba wa viatu
Fontaine
Je,anaikumbuka mechi ipi ya kombe la dunia?
Anaikumbuka mechi ya nusu fainali dhidi ya Brazil hasa tukio la nahodha wao Robert Jonquet kuvunjwa mguu na kiungo wa Brazil Vava.Fontaine anaamini kungekuwa na sheria ya substitution miaka ile basi Brazil wasingeshinda kirahisi mchezo ule.Katika mchezo huo Ufaransa iliwabidi wacheze pungufu sehemu kubwa ya mchezo huo.Huyu ndiye Just Fontaine aliyekuwa na wastani wa bao 1.43 kwa kila mchezo.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top