AJABU NA KWELI, TAZAMA PICHA/VIDEO YA ROBOT LA KWANZA LENYE MOYO NA UWEZO WA KUSOMA HISIA ZA MWANADAMU

Pepper Robot
Kampuni ya Soft Bank ya nchini Japan imetengeneza Robot ambayo ina uwezo ya kuwasiliana na kusoma hisia za mwanadamu.
Pepper Robot
Robot hiyo iliyopewa jina la Pepper inadaiwa kuwa ina uwezo wa kufikiri kama mwanadamu na kufanya kile mtu atakachomwambia na uwezo wa kufanya shughuli mbalimbali kama binadamu.
Pepper Robot
Pepper mwenye urefu wa futi nne ni Robot ya kwanza yenye moyo ambapo ina uwezo kutambua sauti, ishara, maneno kupitia programu ya akili bandia iliyofungwa au ‘emotional engine’.
Pepper Robot
Kampuni hiyo imesema kuwa watu wanaweza kuwasiliana na Robot hiyo kama wanavyowasiliana na marafiki na familia na linaweza kufanya shughuli nyingi.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post