Unknown Unknown Author
Title: WALEMAVU WATATU WAKABIDHIWA BAJAJI TOKA KWA DKT. JAKAYA KIKWETE
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Naibu waziri wa Tamisemi Elimu ambae pia ni Mbunge wa Jimbo hilo Kassim Majaliwa akikabidhi Bajaji hizo kwa walengwa Naibu waziri wa ...
Kassimu Majaliwa
Naibu waziri wa Tamisemi Elimu ambae pia ni Mbunge wa Jimbo hilo Kassim Majaliwa akikabidhi Bajaji hizo kwa walengwa
Kassimu Majaliwa
Naibu waziri wa Tamisemi Elimu ambae pia ni Mbunge wa Jimbo hilo Kassim Majaliwa akimkabidhi Bi Nassim Ramadhan Bajaji yake
Kassimu Majaliwa
walemavu waliokabidhiwa Bajaji Saidi Kunamba.Bakari Ndambile na Bi Nassim Ramadhan wakifurahia zawadi hizo

Na Abdulaziz Video, Ruangwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekabidhi pikipiki aina ya bajaj kwa walemavu watatu katika shughuli fupi iliyofanyika katika Kata ya Mandawa wilayani Ruangwa mkoani Lindi

Shughuli ya makabidhiano inatimiza ahadi ambayo Mheshimiwa Rais aliitoa kwa walemavu hao watatu ili kufuatia ahadi aliyooitoa Mwishoni mwa mwaka jana alipokutana nao alipokuwa katika ziara yake mkoani humo kukagua shughuli za maendeleo.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi pikipiki hiyo kwa Niaba ya Rais Kikwete Naibu waziri wa Tamisemi Elimu ambae pia ni Mbunge wa Jimbo hilo Kassim Majaliwa amewaambia walemavu hao kuwa Rais Kikwete amefurahi sana kutimiza ahadi hiyo ili kusaidia kuchangia uchumi wa walemavu hao ili wajiongezee kipato chao.

Aidha Majaliwa aliwaagiza Viongozi wa kata na kijiji kutoa usaidizi wa kutunza na kusimamia matumizi ya bajaji hiyo ili Iweze kuwa salama na walemavu hao kunufaika na msaada wa Rais Kwa Upande Katibu Tawala wilaya ya Ruangwa ,Silvanus Kilowoko alieleza kuhusiana na Msaada huo alieleza kuwa ofisi yake ilipokea fedha za kununulia bajaj hiyo na tayari wamefanikisha kuisajiri kabla ya kukabidhiwa kwa walengwa.

Akitoa shukrani kwa Niaba ya Ya walemavu hao ambao ni Saidi Kunamba.Bakari Ndambile na Bi Nassim Ramadhan , Mwenyekiti wa CCM Wilayani humo Bw Issa Njinjo kwa upande wake alisisitiza juu ya matumizi ya bajaj hiyo ikiwemo kujiongezea kipato.
Kassimu Majaliwa
Wananchi wakishuhudia makabidhiano hayo

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top