Unknown Unknown Author
Title: VIDEO MPYA YA SAUTI SOUL YAFUNGIWA NCHINI KENYA, CHANZO HICHI HAPA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kama wiki moja hivi imepita , kila mtu alikua akiizungumzia video mpya ya sauti sol ya nishike  na kushangaa how hot and sexy kundi hili l...
Kama wiki moja hivi imepita , kila mtu alikua akiizungumzia video mpya ya sauti sol ya nishike  na kushangaa how hot and sexy kundi hili lilivyobadilika na kufanya kitu kipya. Lakini habari ni kwamba video ya sauti sol imefungiwa kwa kua na “pornography”. Hii sio video ya kwanza kufungiwa nchini Kenya kwa kosa kama hili kwani hata video ya P-Unit “You Guy” ilifungiwa kwa kosa hilohilo.

 Kwa mujibu wa muimbaji mkuu wa kundi hilo,Bien Aime , hivi sasa wapo katika mazungumzo na wakili wa kundi hilo kuangalia jinsi gani watawezesha uoneshwaji wa video hii katika vituo vya televisheni.
Hata hivyo msemaji wa kundi hilo, Anyiko Owoko amesema Wakenya ni wanafiki kwakuwa wamekuwa wakipenda kuangalia video za wasanii wa Marekani akiwemo Beyonce ambazo ni chafu zaidi.
“People won’t stop calling me about #NISHIKE ‘ban’. Aint no ban when a video can be viewed on YouTube,” aliuambia mtandao wa Rap Nairobi.
“Most Kenyans are hypocrites. They don’t see a problem with Beyonce’s Drunk in Love video or Kelly Rowland’s Motivation but Sauti Sol’s is too bad. That’s definitely one of the sexiest songs off new album and deserved that video. That said, it’s not for kids but the grown in general. Really love that most Kenyans are liberal enough to accept it. And Channel O and Kiss TV are already playing it,” aliongeza.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top